Mshambulizi
wa England, Wayne Rooney anahitaji kufunga bao moja tu ili kufikia
rekodi ya ufungaji mabao ‘ wa muda wote’ katika kikosi cha ‘ The Three
Lions’. Mshambulizi wa zamani wa ‘ Simba Watatu’ Gwiji Sir Bobby
Charlton alifunga mabao 49 rekodimbayo haijapata kufikiwa. Miaka lifunga
moja yakumi iliyopita, Michael Owen alionekana kama mchezaji ambaye
angeifikia rekodi hiyo lakini majeraha yalimfanya kuwa nyuma kwa tofauti
ya mabao tisa.
Nahodha wa England, Rooney ‘ Baba Kai’ alifunga moja ya mabao matano
ya England usiku wa kuamkia leo wakati England ilipochomoza na ushindi
wa kishindo dhidi ya San Marino katika uwanja wa Wembley. Mlinzi wa
kati, Phill Jargierka alifunga bao la kuongoza dakika ya 24 kabla ya
Rooney kufun ga bao la 48 kwa England kwa mkwaju wa penalti.
Danny Welbeck alifunga bao lake la Tatu katika michezo miwili ya
England mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Andros Townsend
alifunga bao la nne dakika ya 72, kabla ya wageni kujifunga bao la tano
kupitia kwa Alessandro Della Valle dakika tano baada ya bao la Townsend. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz