Yanga SC ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar katika
uwanja wa Jamhuri, Morogoro baada ya kulala kwa mabao 2-0, lakini timu
hiyo imemudu kupandisha kiwango chake cha kujituma, umakini na nidhamu
na kufunga mabao manne katika michezo miwili iliyopita ukiwemo ushindi
wa siku ya Jumapili dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani katika uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Yanga ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu katika ligi kuu baada
ya kuichapa, Tanzania Prisons ya Mbeya kwa mabao 2-1 wiki moja
iliyopita, na jana wakaifunga JKT Ruvu inayofundishwa na mchezaji/kocha
wao wa zamani Fred Minziro kwa ushindi kama.
Michezo yote hiyo ilifanyika katika uwanja wa Taifa hivyo kufanya
mabingwa hao wa zamani kusogea hadi katika nafasi ya Tatu nyuma ya Azam
FC kwa tofauti ya pointi moja, na pointi Tatu nyuma ya vinara Mtibwa
ambao walishinda kwa mara ya Tatu msimu huu katika uwanja wa nyumbani.
Mtibwa imekusanya pointi tisa baada ya kuzishinda Yanga, Ndanda FC na
JKT Mgambo.
Hakuna mshambulizi aliyefunga bao hadi sasa katika dakika 270 katika
kikosi hicho cha mkufunzi, Mbrazil, Marcio Maximo. Baada ya viungo,
Andre Coutinho na Saimon Msuva kufunga katika ushindi dhidi ya Prisons,
mlinzi Kelvin Yondan alifunga moja ya mabao mazuri hadi sasa katika ligi
kuu wakati alipomnyang’anya mpira mshambulizi, Iddi Mbaga na kuanzisha ‘
move’ aliyopanda nayo hadi alipokutana na pasi ya mwisho kutoka kwa
Haruna Niyonzima. Kelvin alipiga kiufundi mpira akiwa ndani ya eneo la
hatari na kuupeleka pembeni kabisa ya ‘ angle’ na kumuacha golikipa,
Jackson Chove akishindwa la kufanya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Bao la mkwaju wa adhabu ndogo lililofungwa na Niyonzima lililkuwa bao
la nne kufungwa na mchezaji wa nafasi ya kiungo, na lilikuwa bao la
pili ambalo Yanga wamelifunga kwa mtindo huo msimu huu. Hiyo ni mbinu
bora zaidi ya kusaka ushindi kwa timu iliyokamilika kiufundi. Maximo
anawategemea Coutinho ambaye alifunga kwa mpira wa faulo dhidi ya
Prisons, Nizar Khalfan, Niyonzima na wakati mwingine Mrisho Ngassa
katika majukumu ya upigaji wa mipira iliyokufa. Kama faulo itapigwa
upande wa kushoto mara nyingi anapiga, Niyonzima wakati ile ya upande wa
kulia huwa hatari ikipigwa na Coutinho.
Nizar alikaribia kufunga kwa mtindo huo katika mchezo wa Ngao ya
Jamii dhidi ya Azam FC alipopiga kiki ya chini chini nje kidogo ya eneo
la mita 18. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Jabir Aziz Stima alifunga bao la umbali wa zaidi ya mita 20 katika
dakika ya mwisho ya mchezo. Hilo ni bao la nne kwa safu ya ulinzi ya
Yanga kuona likitinga katika nyavu zao katika michezo mitatu iliyopita.
Maximo ana furaha na kiwango kilichoonyeshwa na kinda, Edward Charles
katika michezo miwili iliyopita wakati mchezaji huyo wa zamani wa JKT
Ruvu alipokuwa mbadala wa Oscar Joshua katika nafasi ya beki-tatu,
Charles aliumia dakika kumi tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, na ‘
kiraka’ Salum Telela aliingia kuchukua nafasi yake na kutimiza majukumu
yote ya mlinzi wa kushoto.
Telela amecheza dakika 35 za kwanza katika ligi kuu Bara baada ya
mwaka mmoja. Mechi ya mwisho kucheza ilikuwa ni ile ya sare ya kufungana
bao 1-1 na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine, Mbeya msimu uliopita.
Yanga haina mapungufu makubwa katika ngome lakini ni wakati wa
kujiandaa kuwa na mbadala wakati majeraha yatakapohamia katika safu ya
ulinzi wa kati.
Hakuna hofu sana kwa kuwa Mbuyu Twite anacheza nafasi ya kiungo wa
ulinzi hivi sasa ili kufanya mifumo ya Maximo kuwa na nguvu katika eneo
hilo muhimu ndani ya mchezo. Mbuyu ni mlinzi mahiri hivyo kwa maana
nyingine Maximo anapaswa kurekebisha baadhi ya mbinu zake za ukabaji
kuanzia nusu ya uwanja kuelekea eneo la timu yake.
Yanga inapoteza umakini inaposhambuliwa hilo ni jambo la kawaida
katika mchezo lakini dhidi ya Mtibwa, Prisons na JKT Ruvu bila shaka upo
ulazima wa wachezaji wote kushirikiana uwanjani kuzuia wakati
wanapopoteza mpira.
Kama unawaruhusu wapinzani kujipanga na kupanga mashambulizi kwa
walau dakika tatu bila shaka utakuwa hatarini na ndicho ambacho
kimeonekana kwa Yanga katika michezo mitatu iliyopita.
Yanga inawachezesha timu wengi kiasi cha kufanya mchezo wao kuwa
mzuri na wa kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo. Hassan Dilunga
ametokea kuwa mchezaji wa aina yake katika kikosi cha Maximo, licha ya
kipaji chake cha kumiliki mpira, kupiga pasi na kuichezesha timu, kiungo
huyo amekuwa akicheza kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kiasi
cha kushiriki katika uandaaji wa mabao mengi ya Yanga.
Dilunga, Niyonzima, Coutinho ni safu bora ya mashambulizi lakini bado
hakuna pasi nyingi za mwisho licha ya timu kutengeneza nafasi. Yanga
haijakamilika sana lakini katika michezo mitatu iliyopita imeonyesha
kuwa timu hiyo ina watu watulivu na walio tayari kucheza mpira na
kukubali matokeo huku wakipambana kushinda kila mchezo. Ligi ni ngumu,
City tayari wametoa sare mara mbili wakati Simba imefanya hivyo mara
tatu katika uwanja wa nyumbani.
Yanga wataongeza ‘ gia’ polepole lakini itapanda zaidi wakati wa ‘
Dar- Pacha’ dhidi ya Simba ‘ iliyochoshwa na sare’. Licha ya kufungwa na
Mtibwa, Yanga waliuonyesha uvumilivu, uhitaji wa matokeo, nidhamu, na
sasa wanatakiwa kuendelea kupandisha kiwango chao cha umakini.
Mbinu gani anatumia Marcio Maximo, yeye ni Mbrazil, nitakwambia
wakati mwingine, natafuta Mwalimu wa kumfananisha naye na kuwaambia kwa
nini Yanga itamfunga Simba katika mchezo ujao. Yanga wanashinda mechi
bila washambuliaji kufunga mabao. Katika timu kila mchezaji ni mfungaji. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Baraka Mbolembole
No comments:
Post a Comment