Katika Mashindano ya mbio za
magari ya langa langa ya Formula One dereva wa Ufaransa, Jules Bianchi,
yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuumia vibaya kichwa
chake kutokana na ajali ya kugongana na dereva mwingine katika
mashindano ya Japan Grand Prix. Madaktari wa upasuaji wanaendelea
kumhudumia dereva huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alipoteza fahamu
wakati alipofikishwa hospitalini hapo.Bianchi alipoteza uelekeo wa gari
lake kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, hata hivyo ajali hiyo
iliyosababishwa na mwendo kasi mkubwa.Dereva wa Uingereza Lewis Hamilton
alitangazwa mshindi katika mashindano hayo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment