Wanajeshi
wa Somalia wakisaidiwa na vikosi vya Muungano wa Afrika kwa sasa
wamechukua udhibiti wa mji wa Barawe ambayo ni ngome ya mwisho ya
wanamgambo wa al-Shabab.
Wanajeshi hao waliingia mji wa Barawe
ulio kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu siku ya Jumatatu baada ya
kuuzingira tangu siku ya Jumapili.Sauti za risasi zilisikika mapema Jumatau wakati wanajeshi walikuwa wakiingia mji huo. Ripoti zinasema kuwa kwa sasa mji huo umetulia na magari ya kijeshi kwa sasa yanapiga doria.
Mji wa Barawe haujakuwa chini ya serikali kwa miaka 23 na umekuwa chini ya udhibiti wa al Shabab kwa miaka sita iliyopita.
Gavana na maafisa wa kijeshi waliwahutubia wenyeji leo ambapo walitoa wito wa kuwepo kwa utulivu wakisema kuwa nyakati za al-Shabab zimekwisha.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay alipongeza jeshi hilo la pamoja na kusema kuwa sasa Somalia ina mazuri siku za usoni.
Kutwaliwa kwa mji huo ni pigo kwa kundi la al-Shabab lililo na uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.
Al Shabab wamekuwa wakiutumia mji huo kupitisha silaha na chakula na pia kama kituo cha biashara ya makaa.
Muungano wa Afrika pia unasema kuwa al-Shabab waliutumia mji wa Barawe kupanga mashambulizi yao dhidi ya mji mkuu Mogadishu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment