Masalia ya ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited iliyoanguka katika
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuua watu watatu jana.
Ndege ya Kampuni ya Safari Express
Limited imeanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwateketeza
watu watatu waliokuwamo ndani.
Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka
kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumapili saa 1:26 usiku ikielekea
Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako ilitakiwa kutua saa
2:36 usiku.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(Tanapa), Paschal Shelutete alikiri ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi
hiyo na walikuwa katika harakati za kuitafuta.
Mkaguzi Mkuu wa Ajali za Ndege nchini, kutoka
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, David Nyamwihura alisema ajali hiyo
ilitokea takriban maili 20 kutoka Serengeti, katika eneo la Kogatembe na
watu wote watatu waliokuwamo wamefariki dunia.
Meneja wa Udhibiti wa JKIA, Clever Davor
aliliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kuwa ndege hiyo ilipoteza
mawasiliano na rada ya uwanja huo ikiwa imeruka angani urefu wa futi
14,000. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz