Kaimu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda
alisema jana: “Mawaziri na manaibu ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba walioko mjini Dodoma wanapokuwa na safari za kikazi huaga kwa
Waziri Mkuu lakini jambo la kushangaza ni kuendelea kulipwa posho wakati
hawapo.”
Alisema hali hiyo husababisha Bunge hilo kuendelea
kuwalipa posho kupitia akaunti zao za benki lakini wakiwa hawapo Mjini
Dodoma. Mwakagenda alisema mawaziri hao wanapotoka kwenda kwenye
shughuli mbalimbali za kiserikali nako hulipwa posho. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma,
mawaziri na manaibu wanalipwa posho hata wanapokuwa nje ya Bunge Maalumu
la Katiba, wanaposafiri pia wanalipwa posho na Serikali,” alisema
Mwakagenda.
Alisema pamoja na kwamba Ofisi Katibu wa Bunge
Maalumu la Katiba imeonyesha kubana mianya kwa wajumbe kusaini bila
kufanya kazi, bado kuna ufujaji wa fedha eneo la mawaziri.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis
Hamad alisema ruhusa za kutoka nje ya Dodoma hutolewa na Mwenyekiti wa
Bunge hilo, Samuel Sitta na kwamba wasiohudhuria huwa hawalipwi.
“Tunalipa wajumbe wanaohudhuria bungeni, kama hilo
linatendeka lazima nilifuatilie. Ninachosema kama kuna waziri amelipwa
na hayupo itabidi aturejeshee hiyo fedha. Lakini hili tatizo ni gumu kwa
sababu mtu analipwa na tunajua yupo kumbe pengine hajaingia katika
vikao,” alisema.
Alisema kanuni za Bunge hilo zinataka mjumbe anapoondoka aombe ruhusa kwa Mwenyekiti wa Bunge na nakala kwa Katibu.
“Wakicopy (wakinakili) kwangu mimi nawaorodhesha
nampelekea mhasibu, tukikaribia kulipa namwambia hawa hawapo, kwa hiyo
mtu siku ambazo anaomba ruhusa hata kama anaumwa hatumlipi, labda awe
amelazwa hospitali ambaye tunamlipa half (nusu),” alisema.
Hata hivyo, alisema tatizo linalowapa shida
kiutendaji ni kwa wale wasioaga wanapotoka nje ya Dodoma na kwamba hilo
atalifuatilia kwa kuangalia orodha za mahudhurio kwenye vikao.
Mahudhurio hafifu
Kuhusu mahudhurio Hamad alikiri kwamba hilo ni
tatizo kutokana na baadhi ya wajumbe kutokuwa makini na kwamba
mahudhurio hafifu yanaathiri uendeshaji wa vikao hivyo.
“Kama leo nilikwenda katika kamati nikawaambia kama haupo ni
haupo tu, wengine wakasema unajua wengine walikuwa wanaumwa, nikawaambia
mimi najua hiyo ni luck of seriousness tu (kukosekana kwa umakini),
hakuna lingine. Wakanitaka niombe radhi lakini mimi nikawaambia wala
siombi radhi... Umakini mdogo... Unakuta wengine wanajadili na wengine
wanaathiri kura kwa uzembe tu, nafikiri kama kila mtu angekwenda katika
vikao tusingekuwa na shida.”
Mwakagenda alisema katika wiki mbili zilizopita, mahudhurio yamekuwa madogo katika vikao vya kamati za Bunge.
Alisema Bunge hilo limesema wajumbe 441
wanahudhuria vikao hivyo lakini uchunguzi wa Jukata umeonyesha baadhi
yao wamekuwa wakisaini tu kitabu cha mahudhurio.
Mwakagenda alisema uchunguzi huo ulionyesha kwamba wajumbe 100 hawahudhurii kwenye kamati.
Aidha, alisema kitendo cha Bunge hilo kuendelea
kupokea maoni ya makundi mbalimbali ya kijamii ni kwenda kinyume na
Sheria ya Mabadiliko ya Kifungu namba 9 (1) ambacho alisema kinaeleza
kwamba kazi ya kukusanya maoni ni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment