Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa limepitisha azimio linalotoa wito wa kusitisha mapigano nchini
Libya haraka iwezekanavyo na kuweka vikwazo dhidi watu wanaohusika na
ghasia zinazoendelea nchini humo kati ya makundi ya wanamgambo
wanaopingana.
Balozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa ameliita
azimio hilo kama "msingi", lakini ameonya kuwepo kwa vita vya wenyewe
kwa wenyewe.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshtushwa na kuongezeka kwa mapigano katika ya makundi ya wanamgambo na vikundi vya kijeshi.
Mapigano ya karibuni yamejikita katika uwanja wa ndege wa kimataifa, Tripoli, ambao kwa sasa unadhibitiwa na wanamgambo kutoka Misrata na miji mingine yakiwa chini ya mwavuli wa "Mapambazuko ya Libya", ikiwa ni pamoja na makundi mengine ya kiislam. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Pia Libya inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa, kwa viongozi wawili wanaopingana na mabunge ambayo yanaendesha shughuli zao katika sehemu mbili tofauti za nchi, kila bunge likiungwa mkono na makundi ya wanamgambo wenye silaha.
Uzuiaji wa silaha waimarishwa
Jumatano, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja walipitisha azimio ambalo linatishia kuwawekea vikwazo, kama vile utaifishaji wa mali, kuzuia safari dhidi ya viongozi wa makundi ya wanamgambo na wafuasi wao.
Marekani imeishutumu Misri na Muungano wa Falme za Kiarabu kwa kufanya mashambulio ya anga yakilenga vikundi vya wanamgambo vyenye uhusiano na wapiganaji wa Kiislam.
Azimio hilo limesema kuwa vikwazo vitawalenga watu binafsi na makundi yanayohatarisha usalama wa Libya au kupuuza mageuzi ya kisiasa nchini humo.
Pia azimio limeimarisha upigaji marufuku silaha, amri ambayo tayari imewekwa ambapo mtu au kundi anayetaka kuingiza silaha Libya atahitaji idhini ya mauzo yoyote ya silaha au kibali cha kusafirisha silaha kwenda nchini humo.
No comments:
Post a Comment