Unaweza kushtushwa na umri mdogo wa mtoto mwenyewe
aliekua anafundishwa kufyatua risasi kwenye bunduki, hii imetokea
Arizona nchini Marekani ambapo mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari
kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun iliyotengenezwa Israel.
Mtoto
huyu wa kike anaetokea New York alikua kwenye mapumziko na matembezi
kama mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio alichukua time yake ya
ziada kujifunza kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya risasi
ikafyatuka na kumjeruhi mwalimu wake aitwae Charles Vacca mwenye umri wa
miaka 39 ambae alifariki baadae hospitalini.
Wakati
tukio linatokea mtoto huyu alikua na wazazi wake ambapo tovuti ya
bullets and burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na 17 wanaweza
kufyatua risasi kama iwapo tu watakua chini ya uangalizi wa Mzazi au
Mwalimu.
Hii
sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili, ilishawahi kutokea mwaka 2008
ambapo mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya kwa risasi kwenye
onyesho la bunduki hukohuko Marekani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment