Wanajeshi wa Mreakani wamefanya
mashambulizi ya angani dhidi ya msafara wa magari ya mmoja wa viongozi
wa kundi la Al Shabaab nchini Somalia.
Haijulikani ikiwa kiongozi wa kundi hilo, Ahmed
Abdi Godane aliuawa kwenye shambulizi hilo lililofanyika umbali wa
kilomita 240 kusini ya mjini mkuu Mogadishu.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wanajeshi wa
Marekani walionekana wakishuka katika eneo hilo kwa helikopta na
kuchukua miili ya wapiganaji waliouawa.
Msemaji wa idara ya ulinzi ya Marekani, (Rear Admiral John Kirby) alisema bado inadurusu matokeo ya shambulizi hilo.
Baadhi ya taarifa zinasema kuwa wapiganaji waliwakamata wakazi walioshukiwa kutoa taarifa kwa Marekani.
Na BBC
No comments:
Post a Comment