Umoja wa machifu nchini juzi uliwasilisha mapendekezo yao katika Bunge la Katiba ukitaka yaingizwe kwenye Katiba inayotungwa.
Machifu hao wamependekeza kurudishwa kwa utawala
wa Kichifu na Kitemi ili kutoa nafasi ya kurekebishwa kwa jamii ambayo
kwa maoni yao imeanza kupoteza mwelekeo.
Mapendekezo ya viongozi hao wa jadi, yalipokelewa
na makamu mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan ambaye
aliwaahidi kuyafanyia kazi.
Wakizungumza mbele ya vyombo vya habari jana,
Chifu John Mgemela wa Magu na Agnes Ntuzu wa Bariadi, walisema maoni
hayo yalitokana na mapitio ya Rasimu ya Katiba inayoendelea kuboreshwa
na Bunge hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Tunataka Katiba ieleze wazi kuwa sera na sheria
zitakazotungwa zihakikishe kunakuwa na tume ya taifa ya utamaduni
itakayoanzishwa kisheria kusimamia masuala ya utamaduni,”a lisema Chifu
Mgemela.
Alisema ni vyema Katiba ijayo ikatoa fursa kwa
machifu na watemi kutambulika katika mfumo rasmi wa uongozi wa jamii,
ili wasaidie kudhibiti mwenendo wa jamii ambao kwa sasa umepoteza
mwelekeo kimaadili.
Akipokea mapendekezo hayo, Suluhu alisema ingawa
Bunge hilo halifanyi kazi ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya
kukusanya maoni, hawawezi kukataa kuwapokea wananchi wanaopeleka
mapendekezo yao.
Alisema muda mfupi baada ya kukutana na machifu
hao, ratiba ilikuwa inaelekeza kuwa kamati ndogo ya uongozi wa Bunge
hilo ikutane na miongoni mwa kazi ambazo zingefanywa ni kujadili
mapendekezo yaliyopokelewa.
Alisema ikiwa mapendekezo hayo yatakubalika, maoni
hayo yatawasilishwa kwenye kamati zote za Bunge hilo zinazoendelea
kupitia na kujadili Rasimu ili yafanyiwe kazi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz