Rais
Mohamed Morsi aliepinduliwa madarakani nchini Misri July 2013 amesema
alitekwa nyara na wanajeshi ambao ndio walimtoa kwenye madaraka ambapo
kikundi cha wanasheria waliojitolea ambao hawako kwenye upande wa Morsi,
wametangaza hii baada ya kukutana na Morsi gerezani.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum
Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova amesema
mtuhumiwa huyo ni mkazi wa kiwalani walipata taarifa kwa raia wema
kwamba alishiriki kikamilifu kwenye tukio hilo lilosababisha kifo cha
Dakta Sengodo Elibariki Mvungi.
"mnamo
tarehe 12/11/2013 Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kwamba
kuna mtu ambaye amehusika na tukio la mauaji ya Dakta Mvungi na kwamba
kipindi hicho mnamo saa 12 jioni mtuhumiwa alikuwa maeneo ya mtaa wa
Twiga Jangwani akiwa anaangalia Televisheni," amesema Kamishina
Kova. Marehemu Dakta. Sengodo Mvungi.