Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board)
imefungia viwanja saba vilivyokuwa vikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili
kukidhi mahitaji ya mechi za mpira wa miguu.
Uamuzi huo umefikiwa na TPL Board katika
kikao chake cha kwanza kilichofanyika juzi (Novemba 10 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam ambapo pamoja na mambo mengine kilipitia ripoti za mechi za VPL na FDL
katika mzunguko wa kwanza.
Viwanja
vilivyofungiwa na marekebisho yanayotakiwa kufanyika kwanza ili viruhusiwe
kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba (majukwaa yake yamechakaa,
hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji), na Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini
Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo (dressing rooms) havina hadhi).
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya (sehemu ya kuchezea- pitch ni mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha (pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya kubadilishia kutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini Songea (pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya (sehemu ya kuchezea- pitch ni mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha (pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya kubadilishia kutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini Songea (pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).
Klabu
ambazo timu zake zinatumia viwanja hivyo zimeshaarifiwa rasmi juu ya uamuzi huo
ambapo ama vinatakiwa kuwasiliana na wamiliki wa viwanja hivyo ili wafanye
marekebisho au kutafuta viwanja vingine vya kuchezea mechi zao.
Kwa
upande wa ripoti za mechi za VPL; Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 na
kupewa onyo kali kwa timu yake ya U20 kutocheza mechi ya utangulizi walipocheza
na Yanga. Pia wanatakiwa kulipa gharama za uharibifu baada ya washabiki wao
kuvunja kioo cha basi la Yanga baada ya gharama hizo kuthibitishwa na Bodi ya
Ligi.
Pia
Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kushambulia basi la
wachezaji wa Tanzania Prisons baada ya mechi dhidi yao, na kulipa gharama za
uharibifu baada ya kuthibitisha na Bodi ya Ligi.
Coastal
Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake
ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo mwamuzi msaidizi Hassan
Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa mkononi na kichwa, tukio
lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu.
Beki
wa Coastal Union, Hamad Khamis wa Coastal Union amepigwa faini ya sh. 500,000
kwa kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa Azam. Kitendo hicho
kilisababisha refa amtoe nje kwa kadi nyekundu, hivyo atakosa mechi tatu
zinazofuata za timu yake.
Mchezaji
Cosmas Lewis wa Ruvu Shooting alifanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kupiga
kelele wakati mgeni rasmi akisalimia timu na kukataa kupeana mkono na kamishna
kwenye mechi dhidi ya Rhino Rangers, hivyo amefungiwa mechi tatu na kupigwa
faini ya sh. 500,000.
Mtunza
vifaa (Kit Man) wa JKT Ruvu, Selemani Oga aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati
wa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa refa, hivyo
suala lake litapelekwa katika Kamati ya Maadili.
Kocha
Msaidizi wa Oljoro JKT, Fikiri Elias amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa
mechi tatu kwa kumshambulia kwa matusi refa wakati wa mechi yao dhidi ya
Ashanti United. Naye mtunza vifaa wa timu hiyo Elas Justin amepelekwa Kamati ya
Maadili kwa kumshambulia refa kwa matusi ya nguoni.
Simba
wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake wakati wa
mechi dhidi ya Kagera Sugar.
Katika
FDL, mchezaji Ally Mtoni wa Villa Squad amepigwa faini y ash. 200,000 na
kufungiwa mechi tano. Kosa lake ni kujisaidia haja ndogo golini wakti wa mechi
dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa mjini Mtwara.
Kamishna
Paul Opiyo wa mechi ya FDL kati ya Villa Squad na Transit Camp kwa kutokuwa
makini. Katika ripoti yake ameeleza kuwa Transit Camp ilichelewa kufika
uwanjani, lakini hakusema ilichelewa kwa muda gani.
Kocha
wa Polisi Dar es Salaam, Ngelo Nyanjabha na Meneja wa timu hiyo Mrimi Masi
wamepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi tatu kila mmoja kwa kuongoza
kundi la washabiki kumvamia refa wa mechi yao dhidi ya Villa Squad iliyochezwa
Dar es Salaam.
Pia
Bodi ya Ligi imeagiza Polisi waandikiwe barua ya onyo kwa vile wakati waamuzi
wanapigwa walikuwepo lakini hawakutoa msaada kwa wakati.
Kocha
wa Friends Rangers, Kheri Mzozo amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa
mechi sita kwa kosa la kumtukana refa na kutishia kuhamamisha washabiki waingie
uwanjani kufanya fujo kwenye mechi dhidi ya Villa Squad.
Naye
Kocha msaidizi wa timu ya Transit Camp, Haji Amiri amepigwa faini ya sh.
200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kutoa lugha ya matusi kwa mwamuzi wa akida
wakati wa mechi dhidi ya Friends Rangers.
Adhabu
zote zimetolewa kwa mujibu wa kanuni. Pia Bodi ya Ligi imeahirisha kufanya
uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwa Uwanja wa
Kambarage ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi hiyo haikumalizika. Bodi ya Ligi
itakutana tena Jumapili (Novemba 17 mwaka huu).
No comments:
Post a Comment