Wanajeshi na polisi wa Ufilipino
wamepelekwa katika miji ilioathirika na kimbunga kikali kuwahi kuipiga
nchi hiyo ili kudhibiti wizi wa mali unaohatarisha juhudi za kutoa
misaada ya kibinaadamu kwa waathirika.
Zaidi ya watu 10,000 wanahofiwa
kufariki kutokana na kimbunga hicho kwa jina Haiyan kilichopiga kwa
mawimbi mazito na upepo mkali na kusababisha athari kubwa nchini
Ufilipino siku ya Ijumaa, huku mji wa Tacloban ukiwa moja ya miji
ilioathirika pakubwa.
Waokoaji kwa sasa wanajaribu kupeleka
misaada ya chakula na malazi kwa waathirika wa kimbunga hicho katika mji
huo ulio na idadi ya watu 220,000.
Hata hivyo hatua hiyo iliendeshwa kwa
changamoto kubwa kutokana na wizi uliokuwa ukiendelea. Waporaji
walivunja maduka pamoja na kuvamia gari la misaada la msalaba mwekundu
na kuchukua vile vilivyokuwemo ndani.
Baadhi ya waathiriwa ambao ni wafanyabiashara wadogo pia wameripoti kuibiwa kwa televisheni, na mashini za kufulia nguo.
Kulingana na msemaji wa wizara ya ulinzi wa raia nchini humo, Reynaldo Balido, kurejesha usalama na hai ya utulivu katika mji huo wa Tacloban, ni moja ya mambo wanayoyapa kipaumbele.
Baadhi ya waathiriwa ambao ni wafanyabiashara wadogo pia wameripoti kuibiwa kwa televisheni, na mashini za kufulia nguo.
Kulingana na msemaji wa wizara ya ulinzi wa raia nchini humo, Reynaldo Balido, kurejesha usalama na hai ya utulivu katika mji huo wa Tacloban, ni moja ya mambo wanayoyapa kipaumbele.
Akizungumza na shirika la habari la
AFP hapo jana, Andrew Pomeda, aliye na umri wa miaka 36, na mwalimu wa
shule moja ya upili mjini humo, amesema watu kwa sasa wamegeuka kuwa
wahalifu, kwa kuingia katika majengo ya kibiashara kuiba chakula na
mali. Pomeda amesema ana hofu kwamba kwa muda wa wiki moja watu watakuwa
wanauana kutokana na njaa.
Jeshi la Marekani lajiunga katika shughuloi za uokozi
Wakati huo huo, jeshi la Marekani
limeungana na wenzao wa Ufilipino kuendeleza juhudi ya kuwatafuta
manusura wa Kimbunga Haiyan. Siku nne baada ya kimbunga hicho kuikumba
nchi hiyo na kusababisha maelfu ya miili kutapakaa kote barabarani, sasa
waathirika wana mahitaji makubwa ya chakula, maji, matibabu na malazi.
Joan Lumbre-Wilson mkaazi wa mji wa
Tacloban amesema kinachohitajika kwa sasa ni kundi lililojipanga ambalo
litajishughulisha na zoezi la kuondoa miili iliyotapakaa barabarani na
pia kusimamisha wizi mkubwa wa mali ya watu unaoendelea.
Eneo jengine lililoathirika ni mji wa
Samar ambapo Gavana wa mji huo amethibitisha kuuwawa kwa watu 433 na
kusema idadi hiyo huenda ikaongezeka.
Huku hayo yakiarifiwa, watu 10
wanasemekana kufariki, 67 wamejeruhiwa huku wengine 39,000 wakihamishiwa
katika maeneo salama baada ya kimbunga hicho Haiyan kusababisha mvua
kubwa nchini Vietnam, hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki na
katikati mwa nchi hiyo.
Mwandishi:Amina Abuakar/AFP/dpa
No comments:
Post a Comment