Rais
Mohamed Morsi aliepinduliwa madarakani nchini Misri July 2013 amesema
alitekwa nyara na wanajeshi ambao ndio walimtoa kwenye madaraka ambapo
kikundi cha wanasheria waliojitolea ambao hawako kwenye upande wa Morsi,
wametangaza hii baada ya kukutana na Morsi gerezani.
Rais huyu aliepinduliwa anataka kulishtaki jeshi na
anasema hakutakua na utulivu Misri mpaka hawa watu waliompindua
watolewe na wale waliohusika na umwagaji damu za Wamisri watakapowajibishwa.
Kwenye barua aliyoandika, anasema alitekwa nyara na
hawa wanajeshi siku moja kabla ya kupinduliwa rasmi na baada ya hapo
akashikiliwa kwenye kambi ya jeshi kwa miezi minne na baada ya hapo
akahamishiwa kwenye gereza ambalo wanafungwa watu mashuhuri November 4
baada ya kesi kusikilizwa kwa mara ya kwanza kuhusu mauaji ya December
2012.
Mmoja
wa wanasheria amesema Morsi ana mpango wa kushtaki kisheria kikundi
hicho cha wanajeshi kwa msaada wa wanasheria wake hivi karIbuni na mpaka
sasa hajaamua ni wanasheria gani watamsimamia kwenye hii kesi ya
January 8 2014 ambapo Aljazeera wameripoti kwamba kauli nyingine ya
Morsi ni kwamba Mahakama haistahili kusikiliza hii kesi wala haina
mamlaka ya kufanya wanachofanya.
Kwa kumalizia, Morsi ambae aligoma kuvaa sare nyeupe wanazovaa
wafungwa kwenda Mahakamani huku akipaza sauti kwamba yeye bado ni rais
wa Misri na haitambui hiyo Mahakama inayosikiliza kesi yake, amesema
mpaka hapo alipo anajisimamia mwenyewe kisheria.
No comments:
Post a Comment