“Kutokana na alichofanyiwa kwa kupigiwa kura bila huku akiwa hajafanya
hivyo tumemwandikia barua IGP tukimwomba amwekee ulinzi (Hamis) kwani
kwa siasa za Pemba (anakoishi Hamis) wanaweza kumdhuru.” PICHA|MAKTABA
Siku moja baada
ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi- Zanzibar, Haji Ambar
Hamis kutoa tuhuma za ‘kupigishwa’ kura ya kupitisha Katiba
inayopendekezwa bila ridhaa yake, uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba
umethibitisha kuwapo kwa dosari hizo.
“Sikuwahi kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye
kupitisha katiba hiyo. Ukweli ni kwamba nimeumia sana na hadi sasa
sielewi hatma ya maisha yangu na usalama wa familia yangu kwa ujumla”
alisema Hamis alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Akizungumzia tuhuma hizo za Hamis, Naibu Katibu wa
Bunge Maalumu la Katiba, Dk Thomas Kashililah alisema: “Kwa taarifa
zetu hakupiga kura siku zote tatu za zoezi hilo. Jina lake katika orodha
ya wapiga kura lilikuwa namba 63 na hakupiga kura.”
Alisema hata hivyo wakati wa kuondoa majina ya
Wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wale ambao
hawakushiriki jina lake lilisahaulika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Tuligundua dosari hiyo na ndiyo maana hatukugawa
vitabu siku ya sherehe, tumerekebisha kwa kuchapa vitabu vipya na
vitakuwa tayari Jumatano.
“Aidha, majina yanayoonekana katika kitabu ukiacha
hilo la Haji lililokosewa majina mengine yapo sawa kwa pande zote mbili
na kwamba majina hayo siyo waliopiga kura tu hata wale ambao
walishiriki, lakini hawakupata fursa ya kupiga kura majina yao yapo
katika kitabu,” alisema Dk Kashililah.
Utata wa kura
Kwa upande wa Zanzibar kura mbili ndizo ambazo
zilipitisha Katiba hiyo inayopendekezwa jambo ambalo wadau mbalimbali
walihoji namna zilivyopatikana theluthi mbili.
Akitangaza matokeo hayo Oktoba 2, mwaka huu
bungeni mjini Dodoma, Dk Kashililah alianza kutoa matokeo ya upande wa
Zanzibar ambako wajumbe wengi walikuwa na wasiwasi kuwa huenda usipate
akidi ya kura 146 iliyotakiwa.
Kwa jumla, kura za ‘ndiyo’ za Zanzibar zilikuwa
ama 147 au 148 na ‘hapana’ ama saba au nane; wakati kwa matokeo ya
Tanzania, wajumbe waliopiga kura walikuwa 335 na kura moja tu ndiyo
ilikataa ibara zote na kura mbili zilichomoza kukataa baadhi ya ibara.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Katibu Mkuu
wa NCCR-Mageuzi, Faustin Sungura alisema, kitendo kilichofanywa na
uongozi wa Bunge hilo kinahatarisha usalama wa Hamis.
“Sitta alimkabidhi Rais Kikwete Katiba
inayopendekezwa batili kutokana na mchakato wake kugubikwa na utata
hususan upatikanaji wa theluthi mbili upande wa Zanzibar, wamepandikiza
majina ambayo hayana uhalali kama hili la Hamis walivyomfanyia sasa
mpaka hapo tunaendelea kutilia shaka uhalali wa theluthi mbili za
Zanzibar. Na kuongeza kuwa;
“Kutokana na hatua hiyo, tumemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kumuomba kumwekea ulinzi kiongozi
wetu, kwani atakaporejea Pemba na siasa za huko zilivyo wanaweza
wakamdhuru kutokana na taarifa kuwa amepiga kura ya ndiyo,” alisema.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso
alipotafutwa kutaka kujua kama barua hiyo imefika hakupatikana na
alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi hakujibu.
“Kutokana na alichofanyiwa kwa kupigiwa kura bila
huku akiwa hajafanya hivyo tumemwandikia barua IGP tukimwomba amwekee
ulinzi (Hamis) kwani kwa siasa za Pemba (anakoishi Hamis) wanaweza
kumdhuru.”
Kuhusu kura za hapana zilizopigwa na baadhi ya wajumbe alisema kitendo kilichofanywa kinakandamiza uwepo wa demokrasia nchini.
“Haiwezekani mtu anapiga kura ya hapana halafu eti
unasema tutajadiliana na hao waliopiga kura ya hapana kuona ni kwa
nini...yote haya wameyafanya ili kuhalalisha kile walichokuwa
wakikitaka,” alisema Sungura.
CUF na mbinu chafu
Siku mbili kabla ya Bunge hilo kupiga kura ya
kuipitisha Katiba inayopendekezwa Septemba 29 mwaka huu, Chama cha
Wananchi (CUF) kilibaini mbinu zilizopangwa kutumika ili kuongeza idadi
ya kura zilizotarajiwa kupigwa kwa njia ya mtandao kuunga mkono Katiba
iliyopendekezwa.
Hatua hiyo ilikuwa ni baada ya Bunge Maalumu
kufanya marekebisho ya kanuni zake ili kuwaruhusu wajumbe waliokuwa nje
ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo waliokwenda Hijja kuipigia kura Katiba
inayopendekezwa.
Chini ya marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya
Bunge, ataruhusiwa kupiga kura ya wazi au ya siri kwa njia ya nukushi
(Faksi) au barua pepe kama itakavyoelekezwa na katibu kwa kushauriana na
mwenyekiti.
Akizungumzia njama hizo, Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama wa CUF, Yusuf Salim Hussein, alizitaja mbinu hizo kuwa ni pamoja
na kuingiza majina ya wabunge wa chama hicho na Chadema kwenye orodha
ya waliopiga kura.
“Taarifa tulizo nazo sisi kutoka huko Dodoma ni
kwamba yatawekwa majina yasiyopungua 10 ya chama chetu na 10 ya Chadema
kwamba wamepiga kura katika njia ya mtandao,” alisema Hussein.
Alisema wabunge na wawakilishi wa chama cha CUF
walikuwa na kikao cha pamoja na kukubaliana kwamba hakuna mjumbe yeyote
atakayepiga kura kwa njia ya mtandao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment