Simba SC itacheza na mahasimu wao Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu
Tanzania Bara siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika michezo mitatu iliyopita Simba haijapata ushindi, huku mahasimu
wao wakiwa na pointi sita katika nafasi ya tatu ya msimamo. Yanga ni
timu iliyokamilika kwa sasa, kwa maana ya kucheza kitimu, umoja na
ushirikiano.
Kabla ya safari ya Afrika Kusini, kikosi cha Simba kimeonekana kukosa
‘ utimamu wa mwili na akili’ kwa maana ya wachezaji wake kucheza mpira
huku wakiwa na mambo yanayowasumbua, umoja, kiwango cha chini kutoka kwa
baadhi ya wachezaji, majeraha, na ufiti wa mchezaji mmoja mmoja, kikosi
cha Patrick Phiri kimekuwa katika ‘ majanga’ hayo, lakini kama, mwalimu
hapaswi kutumia sababu hizo kufungwa na mahasimu wao ambao wanaingia
katika mchezo wa tano mfululizo wakiwa katika ‘ umbo zuri’.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mwaka mmoja uliopita, Kiemba alikuwa mchezaji bora zaidi katika
kikosi cha kocha Kim Poulsen, lakini ghafla kiwango cha mchezaji huyo
kiliporomoka kiasi cha kupoteza nafasi yake hadi katika klabu yake.
Mwalimu, Nooij ameendelea kumuita kiungo huyo mzoefu na Kiemba mwenye
miaka 31 hivi sasa aliweza kuthibitisha kuwa yuko safi baada ya kufunga
huku akiichezesha timu. Nooij alimpanga kiungo huyo kama mchezesha timu
mkuu akitokea katikati ya uwanja.
Alicheza kwa dakika 67 huku akiwa makini, mtulivu na kupiga pasi
zilizofika kwa walengwa, zaidi alikuwa akikimbia uwanjani tofauti na
ilivyozoeleka. Stars ilicheza huku wachezaji wake wakikimbia na jambo
hilo liliupendezesha mchezo wa Kiemba ambaye aliweza kupiga pasi nyingi
kuelekea
Marcio Maximo kocha wa Yanga anaitegemea zaidi safu yake ya kiungo
katika kushambulia na kujihami, lakini, Phiri hajui mahala kwa
kushikilia hadi sasa. Kati ya mambo yanayomuumiza kichwa kocha huyo ni
kumkosa kiungo mshambulizi, Paul Kiongera, lakini bado Phiri anaweza
kurudia rudia mara kadhaa video ya mchezo wa jana kati ya timu ya Taifa
ya Tanzania, Taifa Stars na Benin anaweza kupata sehemu ya kuanzia.
Achana na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na Haroun Chanongo katika
mchezo wa jana, kiungo wa mashambulizi, Amri Kiemba alikuwa katika ubora
wa juu. Je, kiwango cha Kiemba dhidi ya Benin kilikuwa na maana gani?.
Anapokuwa fiti kimwili na kiakili, Kiemba ni mmoja wa viungo bora zaidi
wachezesha timu wa Kitanzania, lakini ameshuka kiwango katika kipindi
cha miezi ya karibu kabla ya kiwango cha aina yake hapo jana.
Phiri atakuwa na furaha sasa kwa sababu mechi kati ya timu hizo kubwa
nchini huwa inahitaji wachezaji wazoefu walio fiti. Kiemba ameonesha
kukimbia bila maumivu, ameonyesha ni mchezaji mzoefu mwenye nguvu, akili
ya mpira, na mfungaji wa mechi ‘ maalumu’.
Kiwango chake ni kama kimefikisha ujumbe kwa mwalimu wake kuwa
anaweza kufanya vizuri akicheza na Piere Kwizera, Shaaban Kisiga, Said
Ndemla, Jonas Mkude au mchezaji yeyote Yule ambaye atapaswa kucheza naye. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment