Katibu Mkuu wa CUF,
Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake kitazunguka nchi nzima
kupiga kampeni ili wananchi waikatae Katiba Inayopendekezwa.
Alisema watafanya hivyo kwa kuwa Katiba
iliyopendekezwa imepoteza uhalali kwa vile theluthi mbili (ya wajumbe wa
Zanzibar) inayodaiwa kupatikana haiwiani na takwimu za wabunge
waliokuwamo ndani na nje ya Bunge na wale waliopiga kura ya hapana na
kuwataka wananchi kuikataa wakati ukifika.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza
Zanzibar, alisema hayo jana akihutubia mkutano wa hadhara wa kwanza
tangu Katiba hiyo inayopendekezwa kukabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete na
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ikipendekeza mfumo wa Muungano
wa serikali mbili badala ya tatu kama ilivyokuwa imependekezwa na rasimu
iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na iliyokuwa Tume ya
Marekebisho ya Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Alisema kwa kutumia uwezo wake wa kisiasa na mbinu
nyingine, atahakikisha anawashawishi wananchi kupiga kura ya hapana ili
kuipinga kwa vile haina masilahi kwa Zanzibar.
“Imelenga kupunguza mamlaka kamili ya Zanzibar ya
kikatiba na nawashangaa wabunge wa CCM walioacha kujadili Rasimu ya Jaji
Warioba na kutunga rasimu yao na kuipitisha wao wenyewe na baadaye
kucheza ngoma wakati rasimu hiyo imemeza mamlaka ya Zanzibar,” alisema.
Hata hivyo, alisema hafikirii kujiuzulu wadhifa wake wa Makamu wa Rais licha ya kutoridhishwa na mchakato wa huo.
“Nitaendelea kushika wadhifa wangu wa Makamu wa
Rais, tutabanana humuhumu, nitatetea mamlaka kamili ya Zanzibar nikiwa
ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kamwe sitajiuzulu, hadi
uchaguzi mkuu wa mwakani, tutakapoishika wenyewe Serikali ya Umoja wa
Kitaifa” alisema Maalim Seif. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment