Poland imeifunga UJerumani
kwa mara ya kwanza na kukwea juu ya kilele katika kundi la Nne kuwania
nafasi ya kufuzu kwa fainali za Ulaya, Euro, 2016 nchini Ufaransa.
Mabingwa wa dunia , Ujerumani ilikuwa na rekodi ya kucheza mara 18
mfululizo bila kupoteza mchezo wowote dhidi ya majirani zao, Poland
ambao walipata mabao yote mawili katika kipindi cha pili.
Mshambulizi kinda wa klabu ya Ajax Amsterdam, Arkadiusz Milik, 20
alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 51, na dakika mbili kabla ya
kumalizika kwa mchezo, Sebastian Mila aliwahakikishia wenyeji ushindi
baada ya kufunga bao la pili katika mchezo huo uliopigwa jijini, Warsaw.
Mabingwa hao wa sasa wa dunia, walifungwa mara ya mwisho na Jamhuri
ya Czech, Oktoba, 2007 katika michezo ya kufuzu. Ujerumani ilicheza
michezo 33 ya kufuzu pasipo kupoteza. Kipa wa Ujerumani, Manuer Neur
aliokoa mabao manne ya wazi katika mchezo ambao walishambuliwa sana.
Poland iliyokuwa na mshambulizi wa Bayern Munich, Robert Lewandowski
ilipiga jumla ya mashuti 19, huku mashuti 12 yakilenga bao.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alikwenda Poland huku baaddi ya
wachezaji wake muhimu wakikosekana. Ujerumani ilibanwa hasa na walimudu
kufanya mashambulizi machache . Walipiga mashuti saba tu ambayo yote
yalilenga lango lakini nyota wa mchezo huo, golikipa, Wojciech Szczesny
alikuwa imara, kipa huyo wa klabu ya Arsenal aliokoa mara 14. Tomas
Mueller, Andre Schurrle na Mario Gotze walishindwa kufunga kwa muda wote
waliokuwa uwanjani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment