Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta. PICHA|MAKTABA
Idadi ya wajumbe wa Bunge hilo kisheria ni 629 na
wajumbe ambao hawakuhudhuria vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka
huu, wanakadiriwa kufikia 140.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, aliwahi
kukaririwa akiwaeleza wajumbe wa Bunge hilo kuwa fedha zitakazookolewa
zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa zilikotoka.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Katibu
wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad, alisema hakuna pesa zilizobaki na kwamba
waliomba Serikali kuwaongezea fedha za siku nne zilizobakia kabla ya
kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete Jumatano wiki
hii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Sitta alipotafutwa kutoa ufafanuzi wake simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokewa kwa muda mrefu.
Alipoulizwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
ambaye anakaimu uwaziri wa fedha kuhusu maombi ya nyongeza ya fedha,
alisema hajapokea maombi ya nyongeza kutoka katika Bunge hilo na kwamba
hawajapata mchanganuo wa fedha walizopewa awali.
“Hatujapata mchanganuo wa fedha zilivyotumika.
Utakumbuka kuna wabunge ambao hawakuingia. Kwa hiyo tunaamini kutakuwepo
na chenji, kwa sababu haiwezekani kukawa na wajumbe zaidi ya 100
hawakuingia halafu bado fedha ikatumika vilevile,” alisema.
Wabunge wa Bunge hilo walikuwa wakilipwa kwa siku
posho ya Sh300,000, kati ya hizo Sh70,000 zilikuwa ni posho za vikao, Sh
230,00 zilikuwa ni fedha za kujikimu.
Mwigulu alisema kuwa Bunge hilo lilipewa bajeti ya
Sh32 bilioni na kama Rais Jakaya Kikwete angekubali kuongeza siku 24
zingetumika Sh10 bilioni.
Alisema: “Mimi kwa maoni yangu fedha zote ambazo
zitabaki iwe kwenye kura ya maoni ama ingeenda kuwasaidia watoto wa
maskini waliokosa mikopo ya elimu ya juu,”alisema.
Alisema katika kipindi cha mwaka jana wanafunzi wenye sifa ya kujiunga na vyuo vikuu wapatao 12,000 walikosa mikopo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Chukua taswira ya wale watoto wamesomeshwa na
bibi zao na wajane kwa vipesa vya kuokoteza halafu ikafika wakati wa
kujiunga na chuo kikuu akakosa fedha ya mkopo tena sio bure bali ni
mkopo,” alisema na kuongeza:
“Kwa hiyo naamini fedha yote tunayoipata ina umuhimu wa
kuielekeza kule na wenzangu wizarani bado tunaendelea kubana matumizi
ili kila kijana anayefaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu
basi awe na uwezo wa kukopa.”
Alisema hali hiyo anaitambua tangu angali mbunge tu Iramba Magharibi na kwamba yeye asingepata mkopo asingeweza kusoma.
“Mimi nisingepata mkopo, ndoto yangu ndiyo
ingekuwa ni mwisho wake naamini kwamba leo hii nisingekuwa hapa. Sasa
familia za namna hiyo bado zipo,” alisema.
Kwa mujibu wa Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Bara, jumla ya wanafunzi 12,000 ambao walikosa mikopo ya
elimu ya juu mwaka jana na mwaka huu mahitaji ni kwa wanafunzi 28,000.
“Kwa hiyo utaona fedha yoyote inayopatikana si ya
kufanyiwa luxury (si ya anasa), inatakiwa tuwaangalie kwa jicho la
huruma watu hao,” alisema.
Alisema Bunge hilo lilikuwa linajiongezea siku 24 ambazo hazipo katika bajeti.
“Siku 24 zingehitaji zaidi ya Sh10 bilioni.
Niliwatahadharisha kwa kuongeza siku 24, kwa kuondoa siku za mapumziko
ingefanya Bunge liende hadi tarehe 28,” alisema Mwigulu.
Alisema kwanza ilikuwa ni kinyume cha sheria kwa sababu waraka wa serikali (GN) unasema Bunge liishie Oktoba 4, mwaka huu.
“Lakini pili tunaongeza bilioni 10 kwa wajumbe
kupumzika tu. Kwa hiyo angalizo langu ni kuwa mnapoamua siku hizo ziwe
za mapumziko mnaongeza siku 24 haziko katika bajeti,” alisema na
kuongeza:
“Walikataa lakini namshukuru Mheshimiwa Rais
alisema baadaye kuwa Bunge litaishia Oktoba 4. Wakati mwingine ukiwa
mdogo wa umri na mwili watu wanaweza kupuuza mawazo yako hata yakiwa
mazito. Walipuuza kwamba haina shida wajumbe wanatakiwa wasome,”
alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment