Serikali imesema vita vya kupambana na
ujangili vinaonyesha mafanikio katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita
na hakuna taarifa za kuuawa kwa tembo katika Pori la Akiba la Selous.
Waziri wa Maliasili na Utaslii, Lazaro Nyalandu
alisema jana wakati akiaga wanafunzi zaidi ya 100 kutoka China na
Tanzania Makao Makuu ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara)
waliokwenda kutembelea pori hilo kubwa kuliko yote barani Afrika kupata
mafunzo ya uhifadhi.
Alisema baada ya serikali kuvalia njuga suala la
ujangili wananchi wameelimika na sasa wamekuwa wakitoa taarifa za
majangili ambazo zimesaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na ujangili.
“Baada ya Rais Jakaya Kikwete kukerwa na kukithiri
kwa majangili tulianza mapambano na taarifa nilizonazo hadi hivi sasa
kwa kipindi cha miezi mitatu hakuna tembo hata mmoja aliyekutwa
ameuawa,”alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kasi ya uuaji wa wanyama hao kwa ajili ya biashara
haramu ya meno ilikua kwa kasi katika miaka ya karibuni ambapo takriban
tembo 10,000 walikuwa wakaiuawa nchini kwa mwaka.
Waziri Nyalandu aliwaasa Watanzania kushiriki kutokomeza ujangili nchini, kwani maliasili zilizopo ni za Watanzania wote.
na vizazi vijavyo.
Waziri Nyalandu aliishukuru serikali ya China
ambayo imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia sekta mbalimbali za
maendeleo nchini ikiwamo uhifadhi na kwamba ushirikiano huo ni wa muda
mrefu kutokana na waasisi wa nchi hizo Mwalimu Nyerere na Mao Tse Tung.
“Inafurahisha kuwa uhusiano wetu huu umekuwa wa
tangu enzi hizo, ndiyo maana kiongozi huyo wa China alituzawadia hata
reli hii kwa ajili ya kuimalisha uchumi wa Tanzania.
Kutokana na ushirikiano huo Waziri Nyalandu
alisema kupitia wizara yake itaalika wanafunzi 100 kuja kutembelea
vivutio mbalimbali vya utalii na kuelewa umuhimu wa uhifadhi wa
maliasili.
Hali kadhalika aliahidi wanafunzi wa Tanzania
kutembelea China ili nao wapate fursa ya kujua masuala mbalimbali ya
faida ya maliasili na uhifadhi ili kukuza idadi ya watalii kutoka nchi
hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment