Mshambulizi Karimu Benzema
alifunga bao la mapema na akatengeneza lingine kwa kiungo Paul Pogba
katika kipindi cha pili na kuisaidia Ufaransa kuibuka na ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Ureno. RicaRrdo Quaresma alitokea benchi katika
kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Luis Nani katika dakika ya 68,
alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika tisa baada ya kuingia uwanjamni .
Ufaransa ambao ndiyo wenyeji wa fainali zijazo za Ulaya waliifunga
Ureno ambayo ilikuwa na mshambulizi wake mahiri na mchezaji bora wa
dunia, Cristiano Ronaldo katika mchezo uliofanyika jijini Paris. Ronaldo
alipiga mashuti manne katika mchezo huo lakini ni shuti moja tu ambalo
lilikuwa na uhai. Timu zote zilicheza mchezo wa kufanana, Ufaransa
walipiga mashuti 12 sawa na waliyopiga Ureno, lakini wageni walifanikiwa
kupiga mashuti mawili tu ambayo yalimsumbua golikipa, Steven Mandanda.
Eliaguim Mangala, RAfaer Varane, Patrice Evra na Bacary SAgna
walianza katika safu ya ulinzi na wanne hao hawakuwekwa majaribuni na
kikosi kilichopoteza makali cha Ureno. Ronaldo alitoka uwanjani dakika
ya 76 akimpisha Jose Mario alianza sambamba Danny na Nani katika safu ya
mbele lakini watatu hao hawakuwa tishio kwa Ufaransa ambao walicheza
jumla ya faulo 15 katika mchezo huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment