Wachezaji wa Ujerumani wakumpongeza mwenzao Thomas Muller (kushoto) baada ya kupiga hat-trick leo
MJERUMANI Thomas Muller awa
mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja `hat-trick`
kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil baada ya
kuiongoza nchi yake kuilaza Ureno mabao 4-0 usiku huu mjini Salvador.
Nyota huyo wa Bayern Munich
alifunga bao la kuongoza dakika za mapema kwa mkwaju wa penati na kuwapa
mwanzo mzuri katika uwanja wa Arena Fonte Nova wana nusu fainali hao wa
mwaka 2010 nchini Afrika kusini.
Mabao ya Muller usiku huu yalifungwa katika dakika za 12 (penati), 45, 78, na goli lingine lilifungwa na beki wa kati Mats Hummels katika dakika 32 Ureno walipata majanga baada ya mshambuliaji wake wa kati Hugo Almeida na Fabio Coentrao kupata majeruhi, lakini mbaya zaidi walishuhudia beki wao wa kati Pepe akitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati timu yake iko nyuma kwa mabao 2-0 baada ya kumfanyiwa madhambi Muller. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz