Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad, akizindua kamati tendaji za Wilaya za Pemba katika ofisi za CUF Wilaya
ya Chake Chake
Mwenyekiti
wa CUF Wilaya ya Magharibi Unguja Bi. Raisa Abdallah Mussa, akizungumza wakati
wa uzinduzi wa kamati tendaji kwa Wilaya za Unguja katika ofisi za CUF Wilaya
hiyo zilizoko Kilimahewa.
Hassan Hamad, OMKR.
Chama Cha Wananchi CUF kimesema hakitowavumilia
watendaji watakaobainika kuendeleza fitna na majungu ndani ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
ameeleza hayo kwa nyakati tofauti, wakati akizindua kamati tendaji za (CUF) kwa
Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Kwa upande wa Unguja mkutano huo ulifanyika ofisi za
(CUF) Wilaya ya Magharibi zilizopo Kilimahewa, ambapo mkutano kwa Wilaya nne za
Pemba umefanyika ofisi za CUF Wilaya ya Chake Chake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji Wilaya nne za Pemba wakisikiliza
maelekezo wanayopewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Akizungumza katika Mikutano hiyo Mhe. Maalim Seif
amesema chaguzi kwa ngazi za Wilaya sasa zimekamilika na kuwataka watendaji hao
kuendelea kukijenga chama, badala ya kuendekeza fitna na chuki ambazo zinaweza
kuwagawa wanachama.
Katika hatua nyengine Maalim Seif ametangaza rasmi kuwa
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa Mzee Machano Khamis Ali hatogombea tena
nafasi hiyo kutokana na kuzorota kwa hali ya afya yake.
Hata hivyo amesema Chama kitaendelea kumtunza Mzee
Machano kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika kukijenga na kukiimarisha
chama hicho.
“Mzee Machano ni kisima chetu, na tutaendelea kukitumia
hata akiwa nje ya safu ya uongozi wa chama”, alifahamisha Maalim Seif.
Amesema wakati mchakato wa kuchukua fomu kwa ajili ya
uchaguzi wa viongozi wa kitaifa ukiendelea hadi tarehe 10/06/2014, nafasi hiyo
iko wazi na yeyote anayetaka kugombea nfasi hiyo yuko huru kufanya hivyo.
Ameelezea kuridhishwa na jinsi chaguzi hizo
zilivyofanywa kwa uwazi na kupatikana viongozi waliochaguliwa kwa kura nyingi,
licha ya kuwepo upinzani mkali katika baadhi ya Wilaya zikiwemo Wilaya ya Mjini
na Micheweni, ambapo chaguzi za Wenyeviti zililazimika kurejewa baada ya
kukosekana washindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe.
Hamad Massoud Hamad, kwa mara ya kwanza chama hicho kimepata mwenyekiti wa
Wilaya mwanamke ambapo wajumbe wa mkutano mkuu Wilaya ya Magharibi walimchagua
Bi. Raisa Abdalla Issa kuwa Mwenyekiti wao.
Mhe. Hamad Massoud alisema uchaguzi kwa upande wa Unguja
ulikuwa wa aina yake kwani bila ya kutarajiwa wajumbe wa mikutano mikuu Wilaya
za Unguja waliwachagua wajumbe 47 wanawake kati ya wajumbe 94 waliochaguliwa,
na kufanya idadi sawa katika ya wanawake na wanaume wanaounda kamati tendaji za
Wilaya za Unguja. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment