Farida Abdallah (18), ambaye amedumaa kwa miaka 18.
Wazazi wa binti mwenye ulemavu wa viungo na akili, Farida Abdalah (18) mkazi wa Lukobe Juu mkoani Morogoro wameiomba Serikali, wasamaria wema na wadau mbalimbali kumsaidia binti yao huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya rufaa na anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Pia wazazi hao ambao walionekana kuwa na hali ngumu ya kimaisha
Wazazi wa binti mwenye ulemavu wa viungo na akili, Farida Abdalah (18) mkazi wa Lukobe Juu mkoani Morogoro wameiomba Serikali, wasamaria wema na wadau mbalimbali kumsaidia binti yao huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya rufaa na anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Pia wazazi hao ambao walionekana kuwa na hali ngumu ya kimaisha
waliomba msaada wa kupatiwa matibabu
ya viungo na akili kwa binti yao ili aweze kutembea na kujitambua, kwani
kwa sasa binti huyo amekuwa akilala tu kitandani.
Maisha ya binti huyo ambaye umri wake
haulingani na umbo lake yameguswa na watu wengi, kwani amekuwa haongei,
halii, hasikii na wala hajitambui hivyo amekuwa akivalishwa nepi na
kubebwa kama mtoto mchanga.
Akitoa historia ya binti huyo kwa
mwandishi wa habari hizi jana mama mzazi wa binti huyo Mwajuma Abdalah
alisema kuwa Farida alizaliwa mwaka 1996 wilayani Muheza mkoani Tanga na
alijifungulia nyumbani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mwajuma alisema kuwa baada ya kuzaliwa
binti yake hakuweza kulia na siku zilivyozidi kwenda alimuona akiwa na
dalili za kutokuona wala kusikia na ndipo alipompeleka katika kituo cha
Afya cha Sabasaba kilichopo Manispaa ya Morogoro ambako aliambiwa kuwa
mtoto wake anasumbuliwa na tatizo la mtindio wa ubongo.
"Nimehangaika sana na mtoto wangu
baadaye niliamua kumpeleka hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako
alianzishwa mazoezi ya viungo, lakini hakuwa na dalili zozote za kupona
na kutokana na hali ngumu ya maisha nilishindwa kuendelea na matibabu
katika hospitali nyingine kubwa na hivyo nikakata tamaa na nikamshukuru
Mungu," alisema Mwajuma huku akitokwa na machozi.
Hata hivyo alisema kuwa binti yake
pamoja na kuwa na ulemavu amekuwa akisumbuliwa na magonjwa mara kwa
mara, ukiwamo malaria na kifafa. Kutokana na hali ngumu ya maisha mtoto
huyo amekuwa akikosa vyakula bora na hivyo kusumbuliwa na utapiamlo.
Baba mzazi wa binti huyo ambaye naye
anasumbuliwa na ugonjwa wa kiuno, Abdalah Musa alisema kuwa hali yake ya
maisha kwa sasa imekuwa ngumu sana kwani hana kazi ya kudumu wala
biashara na hivyo siku nyingine amekuwa akikosa hata pesa za kumpeleka
hospitali binti huyo anapoumwa.
Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Lukobe Juu,
Joseph Kamanga alisema kuwa taarifa za mtoto huyo alishazifikisha
katika Baraza la Maendeleo la Kata na kwa wadau mbalimbali lakini hakuna
msaada wowote aliowahi kuupata.
Awali maofisa polisi kutoka dawati la
jinsia walipopata taarifa kuhusu ulemavu wa binti huyo, walikwenda
kukagua mazingira ya chumba alichokuwa amelazwa na kuridhika kuwa
alikuwa akitunzwa vizuri na wazazi wake isipokuwa kutokana na hali ngumu
ya maisha baadhi ya mahitaji ikiwamo lishe na matibabu alikuwa
akiyakosa.
Hata hivyo waliwasiliana na Ofisi ya
Ustawi wa Jamii na kumchukua binti huyo na kumpeleka hospitali ambako
anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na kupatiwa matibabu.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya
rufaa mkoani hapa, Rita Lyamuya alisema kuwa baada ya kupata taarifa za
kulazwa kwa mtoto huyo katika hospitali yake amewatuma madaktari
kufuatilia kwa karibu afya ya binti huyo na kupata historia kutoka kwa
wazazi wake kuanzia mimba hadi makuzi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment