1 — Mechi zote za Kombe la Dunia 1930 nchini Uruguay zilichezwa kwenye jiji moja: Montevideo.
2 — Beki wa Sweden, Jan Olsson, alikuwa akivaa jezi namba 2, beki huyo ndiye aliyemdhibiti vilivyo nyota wa Uholanzi, Johan Cruyff aliyekuwa akisifika kwa aina yake ya ugeukaji na kuwatoroka mabeki “Cruyff Turn” kwenye fainali za mwaka 1974, Ujerumani Magharibi.
3 — Gwiji wa Brazil, Pele ni mchezaji pekee aliyetwaa makombe matatu ya dunia akiwa anacheza mwaka: 1958, 1962 na 1970.
4 — Idadi ya wachezaji waliofunga mabao matatu katika mechi mbili za Kombe la Dunia: Mhungary Sandor Kocsis (zote mwaka 1954), Mfaransa, Just Fontaine (1958), Mjerumani, Gerd Muller (1970) na Gabriel Batistuta (moja 1994 na moja 1998).
5 — Mshambuliaji wa Russia, Oleg Salenko ndiye anayeshikilria rekodi ya kufunga mabao matano katika mechi moja ya Kombe la Dunia, wakati Russia waliposhinda 6-1 dhidi ya Cameroon fainali za 1994 nchini Marekani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
6 — Paolo Rossi alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia mwaka 1982 nchini Hispania, alipofunga mabao sita na kuongoza Italia kutwaa taji la tatu.
7 — Ni idadi ya siku ambazo Kombe la Dunia lilipotea baada ya kuibiwa mwaka 1966 nchini England. Mbwa aliyekuwa aikiitwaa Pickles, aliyekuwa akitembea na mmiliki wake kusini mwa London, aliliona kombe hilo likiwa limefichwa kwa kuzungushiwa na magazeti kwenye kichakani wiki moja baada ya kupotea kwake.
8 — Scotland ni nchi iliyofuzu mara nane kushiriki Kombe la Dunia. Lakini katika mara zote nane ilizoshiriki imeshindwa kufuzu kwa raundi ya kwanza.
9 — Ni rekodi ya Mexico ya kufungwa mechi tisa mfululizo za fainali za Kombe la Dunia (1930, 1950-58).
10 — Ni namba ya dakika zilizobaki katika muda wa nyongeza kwenye mchezo wa fainali ya mwaka 2006 nchi Ujerumani wakati Zinedine Zidane wa Ufaransa alipoamua kumpiga kichwa beki wa Italia, Marco Materazzi na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
11 — Ni muda ambao mshambuliaji wa Uturuki, Hakan Sukur alifunga bao katika sekunde 11 dhidi ya Korea. Kusini mwaka 2002, ndio bao la mapema zaidi kwenye historia ya Kombe la Dunia.
12 — Idadi kubwa ya mabao yaliyofungwa kwenye mechi moja katika historia ya Kombe la Dunia wakati Austria ilipocheza dhidi ya Uswisi fainali za mwaka 1954, iliposhuhudia jumla ya mabao 12 yakifungwa katika mchezo huo ambao Austria ilishinda 7-5.
13 — Ni idadi ya timu zilizoshiriki kwenye fainali za kwanza za Kombe la Dunia mwaka 1930 nchini Uruguay.
14 — Idadi ya mabao yaliyofungwa na nyota wa
Ujerumani, Gerd Muller alishikilria rekodi kwa muda mrefu ya kuwa kinara
wa ufungaji kwenye Kombe la Dunia kwa kuziona nyavu mara.
15 — Ni idadi ya mabao ambayo yamefungwa na mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo kwenye fainali tatu za Kombe la Dunia alizocheza mwaka (1998, 2002 na 2006).
16 — Mwamuzi wa Russia, Valentin Ivanov alitoa kadi za njano 16 kwenye mchezo mmoja na kuweka rekodi hiyo, kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Dunaia mwaka 2006, Ujerumani mechi kati ya Ureno dhidi ya Uholanzi.
17 — Umri wa ambao gwiji wa Brazil, Pele alikuwa
mchezaji mdogo zaidi kucheza Kombe la Dunia na kufunga bao, mwaka 1958
nchini Sweden.
18 — Mchezaji wa England, Geoff Hurst ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao matatu kwenye fainali, bao lake kwanza
kati ya matatu aliyoyafunga dhidi ya Ujerumani Magharibi mwaka1966,
alifunga dakika 18.
19 — Lucien Laurent aliifungia Ufaransa bao dakika
ya 19 dhidi ya Mexico mwaka 1930, na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga
bao kwenye michuano hii ya Kombe la Dunia.
20 — Ni fainali za 20 za Kombe la Dunia ambazo zinafanyika
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment