Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiki akisisitiza jambo
wakati wa uzinduzi wa huduma ya kupata hotuba za Marehemu baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika kwenye hotel ya
Double Tree jana. Ili kuweza kupata hotuba za maneno na picha za video
unatakiwa kutuma neno Hotuba kwenda namba 15678, pia unaweza kupata
huduma hiyo kwa kutumia www.simu.tv/nyerere mobile tv. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile Freddie Manento
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push
Media Mobile, Freddie Manento (kushoto) na Mkurugenzi wa Mtendaji wa
Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku wakibadilisha mkataba mara
baada ya kusainiwa katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kupata hotuba
za Marehemu baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika
kwenye hotel ya Double Tree. Huduma hiyo inamwezesha mwananchi kupata
hotuba mbali mbali mbali za marehemu Baba wa Taifa kwa kutuma neno
Hotuba kwenda namba 15678. Pia unaweza kupata huduma hiyo kwa
kutumiawww.simu.tv/nyerere mobile tv.
Wafanyakazi wa kampuni ya Push Media
Mobile na Taasisi ya Mwalimu Nyerere wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kuzindua huduma ya kumwezesha mwananchi kupata hotuba mbali
mbali mbali za marehemu Baba wa Taifa kwa kutuma neno Hotuba kwenda
namba 15678. Pia unaweza kupata huduma hiyo kwa kutumia
www.simu.tv/nyereremobile tv.
Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA watapata fursa ya kuangalia
na kupata hotuba za marehemu Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere
kupitia mpango ulioanzishwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kwa
kushirikiana na kampuni ya Push Mobile Media.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku alisema kuwa wameamua
kuanzisha mpango huo ili kuwawezesha watanzania, waafrika na dunia kwa
ujumla kujua kazi alizozifanya marehemu Baba wa Taifa kwa jamii.
Butiku Alifafanua kuwa ili kuweza
kupata hotuba hizo kupitia simu ya mkononi unatakiwakutuma neno Hotuba
kwenda namba 15678 . Vile vile unaweza kupata picha nyingi zaidi kwa
kuingia www.simu.tv/nyereremobile tv.
Alisema kuwa mpango huo upo kwa njia ya CD na DVD ambazo watanzania wengi wameanza kuzichangamkia kupata nakala.
"Huu ni mpango maalum wa kuhakikisha
kumbukumbu za marehemu baba wa Taifa zinapatikana kiganjani na muda
wowote, tumeingia makubaliano maalum na kampuni ya Push Media Mobile ili
kuendeleza juhudi hizi za kuenzi enzi zake," alisema Butiku.
Alisema kuwa marehemu Mwalimu amefanya
kazi kubwa za kuelimisha kwa kutunga vitabu mbali mbali ambavyo vingi
vimekuwa vikutumika kusaidia mambo mbali mbali ya kisiasa na uchumi.
"Nakumbuka alisema kuwa mawazo haya
yapo kwenye vitabu na kanda mbali mbali, yatumike katika kuchangia
maendeleo ya binadamu, alikuwa mwangalifu sana kwani yamezingatia hali
halisi ya jana na leo, natoa ushauri kwa watanzania kutumia mpango huu
ili kusaidia taifa," alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile
Media Freddie Manento alisema kuwa wameingia makubaliano na Taasisi ya
Mwalimu Nyerere na lengo kubwa ni kurahisisha kupatikana busara za
Mwalimu kwa watanzania wote, ikiwa pamoja na vizazi vya sasa.
Manento alisema kuwa huduma hii moja ya njia ya kuendelea kumkumbuka Marehemu Baba wa Taifa ambaye pia ni muasisi wa Taifa hili.
Alisema kuwa sababu nyingine ya
kuanzisha huduma hiyo ni kuwakumbusha Watanzania, Waafrika na dunia kwa
ujumla busara zake na hasa kwa njia ya hotuba zake ambazo si za kawaida
kwani bado zinaendelea kuzungumzia mambo mbali mbali yanayotokea sasa.
Aliongeza kuwa mpango huo pia
utaendeleza njia nyingine za kuenzi heshima ya marehemu Baba wa Taifa
katika mchango wake wa kulikomboa taifa hili na mpiganaji wa haki za
binadamu duniani.
Alisema kuwa hakuna asiyejua kuwa
marehemu Baba wa Taifa ni mkombozi wa haki za wanyonge na alikuwa mstari
wa mbele katika kupigiania Uhuru wa Tanzania na mataifa mengine katika
bara la Afrika.
Alisema kuwa mchango wake hauwezi
kusaulika na vizazi vilivyopo wakati wa uhai wake na vizazi vipya
vitakuwa na hamu kubwa ya kupata falsafa zake kupitia hotuba mbali mbali
ambazo zimekuwa zikitumika katika nyanja nyingi hapa nchini.
"Ili kurahisisha upatikanaji wa hotuba
hizo, tumeamua kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation na
kuanzia sasa, unatweza kupata hotuba yake kwa njia ya televisheni na
kwa njia ya meseji kwa kupitia simu ya mkononi na kuendelea kumuenzi
marehemu Baba wa Taifa," aliongeza.
Alisema kuwa huduma hii ni ya mara ya
kwanza kutokea hapa nchini ambapo Watanzania watapata fursa ya kuona na
kusoma hotuba ya marehemu baba wa Taifa kwa njia ya mtandao wa simu ya
mkononi.
Mwisho.....
No comments:
Post a Comment