Thursday, December 25, 2014

MAREKANI: IS HAIKUANGUSHA NDEGE YETU

 Wapiganaji wa IS wakibeba mabaki ya ndege waliodai kuidungua huko Syria 
 
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wamesema kuwa waliidungua ndege ya jeshi la muungano ,lakini Marekani inasema kuwa ushahidi uliopo unaonyesha kuwa hilo si kweli.
Jordan ni miongoni mwa mataifa manne ya kiarabu yaliopo katika muungano wa majeshi yanayoungwa mkono na Marekani ambayo yameanzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa IS.
Ndege hiyo aina ya F-16 ni ndege ya kwanza ya jeshi hilo la muungano kupotea katika maeneo yanayodhibitiwa na IS tangu mashambulizi yaanze mnamo mwezi Septemba.
Rubani wa ndege iliodaiwa kudunguliwa na wapiganaji wa IS akamatwa
Picha za IS zinamuonyesha rubani wa ndege hiyo akikamatwa. Wamemtaja rubani huyo kuwa Moaz Youssef al-Kasasbeh. Wakati huohuo Jordan imesema kuwa hasara iliyopata ya kupoteza ndege yake moja ya kivita, katika anga linalodhibitiwa na waasi wa Islamic State, haitayumbisha majeshi yake kuendelea kukabiliana na matendo ya kigaidi.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MARUFUKU YA EBOLA YATOLEWA SIERRA LEONE

Maafisa wa afya wakibeba miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola nchini Sierra leone taifa hilo limetoa marufuku ya siku tatu kazkazini mwa taifa hilo ili kukabiliana na ebola. 
 
Serikali ya Sierra Leone imetangaza siku tatu za marufuku kaskazini mwa taifa hilo, ili kuruhusu jitihada za kukabiliana na kuenea zaidi kwa ugonjwa hatari wa Ebola.
Msemaji wa serikali amesema kuwa maduka na masoko yatafungwa na hakuna magari ya abiria au pikipiki zitakubaliwa kwenye barabara za eneo hilo.
Sherehe za makanisa kuadhimisha sherehe za siku ya Krismasi pia zimepigwa marufuku.
Sierra Leone ni mojawapo ya mataifa ya Afrika magharibi ambayo yalikumbwa pakubwa na ugonjwa huo wa ebola. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MWAMBUSI AISUKA UPYA MBEYA CITY

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi.
 
Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema tatizo kubwa kwa sasa katika kikosi chake ni safu ya ushambuliaji ambayo ameendelea kuisuka ili wafanye vyema Ligi Kuu Bara itakapoendelea.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwambusi alisema vijana wake wapo ‘fiti’ na wana ari mpya ya kurudisha heshima yao kwa mashabiki wao huku akisema kuteleza siyo kuanguka, kwani yalitokea hivi karibuni ndani ya klabu hiyo yamepita na sasa wanakuja kivingine.

“Ukiangalia mechi zilizopita tulipata mabao mawili tu, na raha ya mpira wa sasa ni kufunga mabao mengi, hivyo nimeona ushambuliaji ni tatizo kubwa, lakini tunaendelea na maboresho katika safu hii,” alisema Mwambusi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAXIMO "MKAKATI WANGU UMENIONDOA YANGA"




Kocha Marcio Maximo 


Kocha Marcio Maximo amesema hana kinyongo na uamuzi wa uongozi wa Yanga kumuondoa, ingawa umefuta ghafla mkakati wa kutaka klabu hiyo iendeshwa kwa weledi.

Maximo na msaidizi wake Leonard Neiva walisitishiwa mikataba yao baada ya Yanga kufungwa na Simba 2-0 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe mwezi huu, ikiwa ni takriban miezi mitano tangu aje nchini.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda ndege kurudi kwao Brazil jana, Maximo alisema hana kinyongo na uamuzi huo, lakini akaitaka klabu hiyo kongwe kuendeleza soka la vijana na kutengeneza mindombinu kama inataka kupata mafanikio makubwa katika soka.

Alisema katika muda mfupi aliokuwa klabu hiyo, alijenga misingi ya utendaji kazi wa kisasa ndani na nje ya uwanja kwa wachezaji ili waweze kujitambua katika kazi yao, lakini jambo hilo limeishia njiani. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

PLUIJM NA PHIRI WAJIGAMBA

Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm




Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm na mwenzake Patrick Phiri wa Simba wametamba kuibuka na ushindi dhidi ya Azam na Kagera Sugar wakati mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zitakapoingia raundi ya nane kuanzia kesho.

Pluijm alisema kuwa anaiheshimu Azam FC kama moja ya timu bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, lakini hana hofu yoyote.

“Nawaandaa vyema vijana wangu waibuke na ushindi kwenye pambalo hilo kwa sababu litatuweka kwenye nafasi nzuri nje na ndani ya uwanja,” alisema Pluij
m. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Wednesday, December 24, 2014

PROF. TIBAIJUKA: BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA


Aliekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Siku moja baada ya kufukuzwa  uwaziri, Mbunge wa Muleba Kusini (CCM),  Profesa Anna Tibaijuka amewasili jimboni kwake na kusema, “Bwana alitoa na Bwana ametwaa.”
Profesa Tibaijuka alivuliwa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Rais Jakaya Kikwete juzi kutokana na kuhusika kupokea fedha katika akaunti binafsi.
Baada ya kuwasili na kupokewa kwa maandamano, Profesa Tibaijuka aliwaomba wananchi kukaa kimya kwa dakika moja ili kumkumbuka katibu wake wa jimbo aliyefariki dunia wakati sakata hilo likijadiliwa bungeni.
Profesa Tibaijuka aliyepokewa kwa msafara wa magari kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba, aliwaeleza wananchi kuwa ilikuwa ni lazima kutafuta msaada kwa watu wengi ili aweze kuwasomesha watoto anaowasaidia kielimu.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MASWI ASIMAMISHWA KAZI KWA MUDA

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue naye ametangaza kumsimamisha kazi kwa muda Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Maswi amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais Kikwete juzi wakati anahutubia taifa kupitia wazee na wakazi wa Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

DAKTARI ALIYEKUTWA KALEWA GEITA AVULIWA CHEO


Wagonjwa wakimtia adabu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Nyakabale mkoani Geita, Josephat Msafiri baada ya kuwatelekeza juzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Magreth Nakainga amemvua madaraka Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyakabale, Josephat Msafiri kwa kukiuka miiko ya kazi yake na kulewa wakati wa kazi.
Mkurugenzi huyo aliamua kuchukua uamuzi huo jana kutokana na tukio lililotokea Juzi hii la daktari huyo kufunga kituo cha afya na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa, kisha kwenda kunywa pombe jambo lililowalazima kumchapa viboko akiwa baa.
“Tumeshamchukulia hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka yake ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa Serikali,” alisema Nakainga.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 24, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
DSC07535
DSC07530 
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

RAIS KIKWETE ATA WANAOKIUKA MAADILI KUWAJIBISHWA

Rais Jakaya Kikwete.

 RAIS Jakaya Kikwete 

RAIS Jakaya Kikwete amesema ni lazima watumishi wa umma wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma wawajibishwe ili iwe fundisho kwao na kwa wengine.

Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam juzi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kumkaribisha kuzungumza na wazee wa jiji hilo.
Awali kabla ya Rais kuzungumza, Sadiki katika hotuba yake alimwelezea Rais jinsi Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa ulivyofanyika jijini mwake na kusema CCM imefanya vizuri kwa kuibuka na ushindi wa jumla ya asilimia 75.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

GEORGE BUSH ALAZWA BAADA YA KUPATA TATIZO LA KUPUMUA

 George H.W Bush.
 
Aliyekuwa rais wa Marekani George H.W Bush amekimbizwa katika hospitali moja ya Houston nchini Marekani baada ya kupatikana na tatizo la kupumua.
Kulingana na madaktari,Bush mwenye umri wa miaka 90 anachunguzwa katika hospitali ya Methodist.
Alipelekwa katika hospitali hiyo na ambalensi jumanne usiku.
Wawakilishi wa Bush wanasema kuwa hatua hiyo ya kupelekwa hospitali ni kama tahadhari.
Rais huyo wa 41 ndio mzee kuwahi kuiongoza Marekani akimshinda Jimmy Carter kwa miezi michache.
Alihudumu kwa muhula mmoja baada ya kushindwa na Rais Bill Clinton.
Bush ambaye hawezi kutumia miguu yake,hivi majuzi alionekana amekaa katika kiti cha magurudumo katika hafla iliofanyika mwezi November katika chuo kikuu cha Texas na mwanawe aliyekuwa rais George W Bush. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

EBOLA BADO TISHIO

 Peter Piot 
 
Shirika la Afya Duniani limesema ugonjwa wa Ebola hautaweza kudhibitiwa kikamilifu katika kipindi cha mwaka mmoja unaokuja.
Mwenyekiti kutoka kitengo maalumu kinachoshughulikia ugonjwa huo, kutoka katika Shirika la Afya Duniani Profesa Peter Piot anasema hali halisi kwa sasa ya ugonjwa huo ni kama ugonjwa utakaodumu muda mrefu.
Profesa Peter Piot ambaye amerejea kutoka nchini Sierra Leone, nchi ambayo imeathiriwa zaidi na ugonjwa huo, ameiambia BBC kwamba amehamasishwa na ahadi za kupatikana kwa kinga mpya ambayo inaaminika itakuwa tayari katika kipindi cha miezi mitatu.
Hata hivyo Profesa Piot ambaye aligundua virusi vya ugonjwa wa Ebola mwaka 1976, ameonya pia kwamba janga lililopo sasa halitakuwa la mwishon na chanjo kudhibiti kirusi hicho itachukua muda kufanya kazi. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC Swahili

VILABU VYA ULAYA NA TETESI ZA USAJILI

 Gareth Balle akiwa kazini.
 
Uongozi wa Timu ya Manchester United umesema upo tayari kutoa paundi milioni 120 kwaajili ya kumsajili winga Gareth Balle mwenye umri wa miaka 25 kwa mwezi januari kutoka klabu ya Real Madrid , winga ambaye ni miongoni mwa wachezaji ghali zaidi ulimwenguni.
Gareth Bale alijiunga na Real Madrid kwa kuweka rekodi kubwa duniani kwa usajili wa rekodi ya paundi milioni 85.3 mwaka 2013.
Wakati huo huo kocha Laurent Blanc wa Timu ya Paris St Germain anafikiria kumsajili mshambuliaji Edinson Cavani( 27), kwa gharama ya pauni milioni 50 ikiwa ndio hitaji la Timu ya Arsenal katika katika usajili wa mwezi Januari 2015.
Nayo klabu ya Manchester City inandaa pauni milioni 25 katika jitihada za kutaka kumsajili msahambuliaji wa Atletico Madrid Mario Mandzukic (28). Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

EBOSSE: ALGERIA YAPINGA RIPOTI YA MAUAJI

Marehemu Albert Ebosse aliyeaga dunia.Algeria imepinga ripoti ya mauaji yake kwamba mchezaji huyo aliuawa baada ya kuvamiwa. 
 
Waziri wa habari nchini Algeria Mohammed Tahmi amesisiiza kwamba kifo cha mchezaji wa Cameroon Albert Ebosse kilisababishwa na mashabiki waliokuwa wakirushi vitu.
Tahmi ambaye alikuwa akizungumza na radio ya Algeria alikuwa akijibu ripoti ya wiki jana ya daktari wa kuchunguza mauaji kwamba majereha ya Ebosse yalisababishwa na mashambulizi.
Ebosse mwenye umri wa miaka 25 aliaga dunia tarehe 23 mwezi Agosti baada ya kilabu yake JS Kabylie kupoteza 2-1 nyumbani. ''Tumefanya uchunguzi wetu unaoonyesha kwamba mchezaji huyo aliuawa kutokana na kitu kilichorushwa kutoka kwa mashabiki.'',alisema
Mchezaji Ebose aliyekuwa akiichezea timu yake JC kabylie kutoka Algeria
''Mimi si mtaalamu wa sheria lakini nitasema kuwa kifo hicho ni cha bahati mbaya''.,aliongezea ''Vitu vilirushwa kutoka pande zote mbili na wachezaji wote walilengwa na kwa bahati mbaya kisa hicho kikatokea'',alisema.
Swala hilo kwa sasa liko mahakamani ambapo uamuzi utatolewa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

IVORY COAST WAGOMEA BAJETI YA SERIKALI - AFCON

 Timu ya Ivory Coast 
 
Shirikisho la soka Ivory Coast (FIF) limegomea bajeti waliyopewa na Serikali ya nchi hiyo kwa ajili ushiriki wa timu ya taifa, The Elephants kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kwa sababu ni ndogo.
Serikali imekubali kutoa dola za Kimarekani 575 805 kwa Tembo wa Ivory Coast kwenye Fainali za AFCON zitakazofanyika Equatorial Guinea kuanzia Januari 17 hadi Februari 8.
Pamoja na hayo, Makamu wa rais wa FIF, Sory Diabate amewaambia Waandishi wa Habari kwamba Hawawezi kwenda CAN (Mataifa ya Afrika) na faranga (za Ivory Coast, CFA Francs) Milioni 310. Kwa kuwa wamewasilisha bajeti yao kwa ufafanuzi mzuri.
Waziri wa Michezo wa nchi hiyo alikuwa tayari kutoa fungu kamili waliloombwa katika bajeti ya awali faranga bilioni 3.5, pamoja na hayo Ivory Coast ilikwenda michuano hiyo mwaka 2013 Afrika Kusini na jumla ya Faranga bilioni 3.9, huku Serikali ikichangia Bilioni 2.7 wakati Tembo walitolewa na Nigeria katika Robo Fainali.
Kikois cha Herve Renard, kitaanza maandalizi yake kwa kuweka kambi Abu Dhabi, Falme za Kiarabu Januari 5, mwakani. Ivory Coast imepangwa Kund D pamoja na Mali, Cameroon na Guinea. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...