Libya
imekamilisha uharibifu wa silaha za kemikali katika mpango ulioanza
miaka tisa iliyopita chini ya uongozi wa aliyekuwa rais, Muammar
Ghaddafi.
Tangazo hilo lilipitishwa katika mkutano wa wanahabari uliofanyika Jijini Tripoli na kuhudhuriwa na wajumbe wa kimataifa .
Ikisaidiwa na Marekani, Ujerumani, na Canada, Libya imeharibu shehena ya sumu ya mvuke pamoja na silaha nyengine zenye sumu.
Katika
mkutano huo Katibu Mkuu wa Shirika la Silaha za kemikali zilizopigwa
marufuku amepongeza Libya kwa kuchukua hatua hiyo muhimu.
Amesema kwamba hatua hiyo ni mfano mwema wa ushirikiano wa kimataifa ambao unaigwa na taifa la Syria kwa kiwango kikubwa.
Kwenye
mkutano huo waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya ameeleza kwamba
hatua hiyo ni ya kihistoria na ni mafanikio kutokana na ushirkiano na
washirika wa kimataifa.
Mnamo mwaka wa 2004,Libya ilikuwa na takriban tani 13 za sumu ya mvuke.
Mrundiko huo wa kemikali hatari kwa sasa umeharibiwa.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz