**********
Pamoja na kushindwa kutaja tarehe rasmi ya kuanza kuboresha
daftari la kudumu la wapigakura, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema
daftari hilo litaboreshwa kabla ya kuanza kwa upigaji wa kura ya maoni
kwa ajili ya kupata Katiba Mpya. Upigaji wa kura hiyo utafanyika ndani
ya siku 70 baada ya kumalizika kwa Bunge Maalumu la Katiba
linalotarajiwa kuanza katikati ya mwezi ujao mjini Dodoma. Litafanyika
kwa kati ya siku 70 na 90.
Nec imetoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa
malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wananchi kwamba tangu uchaguzi
mkuu wa mwaka 2010, daftari hilo halijawahi kuboreshwa, jambo ambalo
litasababisha upigaji wa kura kwa ajili ya kupata Katiba Mpya kutawaliwa
na vurugu. Malalamiko hayo yanatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu
waliotimiza umri wa kupiga kura lakini hawamo katika daftari hilo.
Pia waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura na wenye kasoro mbalimbali zinazowafanya wapoteze sifa.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva jana alitoa
taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa tume hiyo imeshapata
fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kuendesha mchakato wa kufanya
maboresho hayo.
“Tumeanza mchakato wa kuboresha daftari kwa kuanza kuhakiki vituo vya uandikishaji wa kupiga kura vitakavyoongezeka kwa lengo la kuvisogeza karibu zaidi na wananchi,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
“Tumeanza mchakato wa kuboresha daftari kwa kuanza kuhakiki vituo vya uandikishaji wa kupiga kura vitakavyoongezeka kwa lengo la kuvisogeza karibu zaidi na wananchi,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Inafafanua kwamba mpaka kufikia upigaji wa kura ya
maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya na uchaguzi mkuu mwaka 2015,
daftari hilo litakuwa limeshafanyiwa marekebisho.
“Nec inawataka wananchi kutokuwa na wasiwasi juu
ya suala hili. Jukumu la kusimamia na kuendesha mchakato huu ni la tume
hii hivyo vyombo vingine visijiingize katika shughuli zisizowahusu”
inaeleza.
Katika taarifa hiyo Nec imevitaka vyama vyote 21
vya siasa nchini kuwahamasisha wananchi kushiriki katika kura ya maoni
na Uchaguzi Mkuu ujao, siyo kuwayumbisha wananchi juu ya suala hilo.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment