Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka amekifungia kwa muda usiojulika shughuli za uzalishaji, Kiwanada cha Sukari cha Mtibwa mpaka kiwanda hicho kitakapolipa madeni ya wafanyakazi na wakulima wa miwa.
Akitoa msimamo wa Serikali ya wilaya
hiyo juu ya kukifungia kiwanda hicho mbele ya wafanyakzi na wakulima hao
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za mtendaji wa kata
ya Mtibwa wilayani hapa, Mtaka alisema, wamechukua uamuzi huo baada ya
mabishano ya muda mrefu baina ya pande mbili kutofikia muafaka.
Mkuu huyo wa wilaya katika mabishano
hayo ya muda mrefu juu ya madai ya wakulima na wafanyakazi alisema
wanakidai Kiwanda cha Mtibwa zaidi ya Sh1.9 bilioni ambazo ni za mauzo
ya miwa na mishahara ya wafanyakazi.
Mtaka alisema shughuli nyingine
kiwandani hapo zitaendelea kama huduma ya afya, ulinzi na idara ya fedha
ili kuwezesha makundi hayo kupata mafao yao mwishoni mwa wiki hii kama
ilivyoahidiwa na uongozi wa kiwanda hicho.
Meneja mkuu Hamad Juma alisema,
kiwanda hicho kilikwama kulipa madeni hayo kutokana na uingizwaji mwingi
wa sukari nchini uliosababisha wao kukosa soko ingawa waliahidi kuanza
kulipa mwezi huu. Chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment