Dar es Salaam. Wakazi
wa Tabata na viunga vyake, sasa wanaishi kwa wasiwasi mkubwa kutokana
na kuibuka kwa kundi la vijana, wanaojiita Mbwa Mwitu wakitumia silaha
za jadi, kujeruhi watu na kupora mali nyakati za usiku.
Mmoja
wa wananchi wa Tabata Matumbi alisema wiki mbili zilizopita, vijana hao
walimuua mwanamume mmoja kwenye Daraja la Reli la Matumbi. Kwa mujibu wa
mtoa habari huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe, mtu huyo
alichinjwa na kichwa chake kutenganishwa na kiwiliwili.
“Watu
walipeleka kiwiliwili kituo cha polisi, maana kichwa hakikupatikana na
haikufahamika kama alitambuliwa au vipi. Yaani sasa hivi ikifika saa
tatu watu inabidi tubaki ndani,” alisema.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Habari zilisema pamoja na mauaji hayo, pia kumekuwa na matukio ya watu kuvamiwa, kujeruhiwa na kuporwa mali zao.
Inasemekana vijana wanaofanya uhalifu huo ni wa umri wa kati ya miaka 14 na 17.
Mtu
mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Pima alisema alivamiwa na kundi
la vijana wasiyopungua kumi akiwa nje ya nyumba yake. Alisema vijana
hao walimkata panga kichwani, baada ya kutotii amri yao ya kutaka
awakabidhi simu na kila alichokuwa nacho mfukoni.
“Kwanza
walipita watoto watatu, wakafuatiwa na wengine watatu, mara akatokea
mmoja na kunifuata barazani, akanitaka nimpe simu, nikahisi anatania
maana ni katoto,” alisema Pima.
Alisema ghafla walitokea wengine wawili na kumwamuru atekeleze amri mara moja.
Alisema
mmoja alijaribu kumpokonya simu, lakini akamwahi. Mtu huyo alisema hata
hivyo kiongozi wao alimjeruhi kwa panga kichwani.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Msimbazi, Beatrice Mukama alisema juzi baadhi ya
wananchi wa kushirikiana na polisi waliendesha msako uliowezesha
kukamatwa kwa watuhumiwa 16 .
Alisema watuhumiwa hao wamekabidhiwa polisi-Bunguruni.
Chanzo: Mwananchi
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment