Kamanda Jacob Mwaruanda. |
Mwili wa
mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne mwenye ulemavu wa ngozi
(albinism) umezikwa ndani ya nyumba ya babu yake mjini Sumbawanga
katika mkoa wa Rukwa badala ya kuzikwa katika shamba la wafu la
Wakatoliki.Tukio
hilo la maziko ya mtoto huyo licha ya kuwa gumzo mjini hapa,
pia lilihudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji.
Uamuzi huo unasadikiwa na wengi kuwa ni hofu kuwa endapo
mwili wake ungezikwa katika shamba la wafu upo uwezekano mabaki yake
kufukuliwa na kunyofolewa viungo vyake na watu wenye imani za
kishirikina.
Mwaka jana watu wawili wenye ulemavu wa ngozi walishambuliwa na
kunyofolewa mikono yao na watu wenye imani za kishirikiana ambao
wanadaiwa kuamini kuwa viungo vya binadamu hao vina uwezo mkubwa
wa kumtajirisha mtu kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Jacob Mwaruanda
watuhumiwa katika visa vyote viwili walikamatwa na mashauri yao
yako katika hatua mbalimbali za kusikilizwa mahakamani.
Baadhi ya waombolezaji walioshuhudia maziko ya mtoto huyo
yaliyofanyika juzi saa kumi na moja jioni walisikika wakisema;
"Tumefarijika mwili wa marehemu kusitiriwa ndani ya nyumba ya babu
yake tulikuwa na hofu sana maana kama angezikwa makaburini baada
ya waombolezaji kuupa kisogo shamba hilo la wafu hakika
ungefukuliwa."
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hapo msibani, mjomba wa
marehemu aitwaye God Mwangamila ' Kizibo' ambaye alikuwa akiishi na
mtoto huyo kuwa aliaga dunia Januari 29, nyumbani kwake mjini hapa
kutokana na ugonjwa wa malaria.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment