Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kwamba Rais Kikwete
amekubali kutengua nyadhifa za mawaziri wanne kufuatia ripoti ya
'Operesheni Tokomeza' iliyotolewa mapema leo bungeni.
Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha wa Ulinzi.
Mhe. Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu.

Endelea kutembelea blog hii ya Jambo Tz kwa habari zaidi. Pia usisahau ku-like page yetu ya facebook click neno Jambo Tz