NCHINI
Afrika Kusini, hakuna eneo la kivutio cha kitalii linalotembelewa na
wageni wengi kama Kisiwa cha Robben. Umaarufu wa eneo hili umekuwa
ukiongezeka mwaka mpaka mwaka.
Lakini
hakuna shaka kwamba, kiini cha kutembelewa sana kwa kisiwa hiki ni
kutoka na kuwa kituo maalumu cha kuwafunga wapigania uhuru wa Afrika
Kusini wakati huo, akiwamo Nelson Mandela.
Mandela,
Rais wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini, ndiye mhimili wa kivutio
cha utalii kwenye jela ya wafungwa wa kisiasa iliyojengwa ndani ya
kisiwa hicho.
Kati
ya wafungwa wengi wa kisiasa waliowahi kufungwa kwenye jela ya Robben,
alikuwamo Govan Mbeki, baba mzazi wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini
aliyempokea madaraka Mandela, Thabo Mbeki. Ni Mandela pekee ndiye
aliyekaa hapo muda mrefu.
Mpiganaji
Mandela aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela, alitumia miaka 17 kwenye
jela hiyo kati ya miaka 28 aliyosota kabla ya kuachiwa huru mwaka 1990.
Kufariki
kwa Mandela wiki iliyopita, kumechochea kwa kiasi kikubwa kuongezeka
umaarufu wa Kisiwa cha Robben kinachoendelea kuwa na historia ya pekee
kwa aina yake duniani.
Jela
ya kisiwa hiki, pia aliwahi kufungwa mwasisi wa Chama cha Pan
Africanist Congress (PAC), Robert Mangaliso Sobukwe na mwanaharakati
mwingine wa ANC, Walter Sisulu.
Mwanaharakati
mwingine aliyekuwa akipinga ubaguzi wa rangi wakati huo, Jeff Masemola
ameweka historia kwa kuwa mfungwa wa kwanza kuhuhumiwa kwenda jela
maisha.
Mbali
na kufungwa Jela ya Robben, Mandela pia alitumikia kifungo kwenye
Magereza ya Pollsmoor (1982–1988) na Victor Verster (1988–1990) kabla ya
kuachiwa huru pamoja na wafungwa wengine.
Rais wa mwisho mzungu Afrika Kusini, F. W. de Klerk ndiye aliyemtoa Mandera katika Gereza la Victor Verster.
Umaarufu
wa Robben Island hauishii hapo tu, kwani kisiwa hicho ni kitovu cha
makazi ya ndege aina mbalimbali zaidi ya 100, wakiwemo ndege aina ya
Penguin wa Afrika wanaofikia idadi ya 140,000.
Kisiwa
hiki chenye historia ndefu tangu wakoloni wa Uholanzi walipoingia kwa
mara ya kwanza katikati ya miaka 1600, kiko umbali wa kilomita 6.9
kutoka Bloubergstrand, Cape Town.
MWANANCHI
Bofya hapa Jambo Tz
No comments:
Post a Comment