Dar es Salaam. Mkurugenzi wa zamani wa
Utawala na Utumishi (DPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba
anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na simu gerezani, ameiomba mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imfutie shtaka hilo na kumuachia huru kwa madai kuwa
kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kumkomoa.
Liyumba aliyaeleza hayo jana wakati
akijitete mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando anayetarajia kutoa
hukumu ya kesi hiyo, Januari 15, mwaka na kuzitaka pande zote mbili
kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho kama mshtakiwa ana hatia ama la,
Desemba 30, mwaka huu.
"Kesi hii imepangwa kwa ajili ya
kunikomoa, wakati natumikia kifungo sijawahi kuvunja sheria, kupewa
adhabu wala kuonywa kwa kosa lolote, simu yenye namba 0653004662 siijui
nimeiona hapa na kama imesajiliwa ni lazima mhusika atajulikana."
alieleza Liyumba.
Alidai kuwa, Julai 2011 alikuwa
mfungwa akitumikia kifungo cha miaka miwili na unapofikishwa huko ni
lazima upekuliwe mara tatu kwa kuvuliwa nguo zote.
Kutokana na utaratibu wa ulinzi gerezani, siyo rahisi kwa mfungwa ama mahabusu kuingia na simu
Julai 27, 2011 mchana nikiwa kwenye
selo yangu na mtu mmoja ambaye ni mahabusu, tukisoma magazeti ghafla
askari wawili akiwamo shahidi wa pili wa upande wa mashtaka, waliingia
na kuniambia kuwa hii simu umeipataje wakati wakiwa wameishika mkononi.
Aliongeza kuwa tukio hilo kwake
lilikuwa ni mshtuko na aliona ni kitu kilichopangwa na kwamba, wakati
huo ilikuwa bado mwezi mmoja na nusu amalize kutumikia kifungo chake.
"Naamini walikuwa wananingojea,
nilitafakari mlolongo wa matukio yanayonikuta, nilishtakiwa kwa kuambiwa
nimesababisha harasa ya Sh261 bilioni shtaka ambalo liliondolewa na
kupewa la kutumia madaraka vibaya, madaraka ambayo sina wala sijapewa
huu ni uonevu." alisema Liyumba.
Alibainisha kuwa wakati akiwa gerezani
muda mfupi kabla ya kutoka watu wa Takukuru walimfuata na wakitaka
kuandaa kesi dhidi yake, lakini aliwapinga kwa madai ya kutaka
kuwasiliana na mwanasheria wake.
Alidai kuwa watu hao walimfuata tena
na kwamba baada ya dulu hilo, akaona tukio hili la Julai 27,2011 la
kubambikiwa kesi ya kukutwa na simu gerezani.
Alisisitiza kuwa simu na namba ya
0653004662 haifahamu, kama imesajiliwa mhusika atajulikana na iwapo
atakuja mtaalamu ataeleza angalau ilipigwa kwa nani.
Liyumba anadaiwa kukutwa na simu ya mkononi akiwa gerezani Ukonga, Dar es Salaam, wakati akitumikia kifungo cha miaka miwili.
Na Tausi Ally, Mwananchi
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu like page ya facebook sasa bofya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment