rubani wa ndege Andreas Daffee. akipongezana na wakili wake Lweikaza |
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mbeya, imewaachia huru watuhumiwa watatu ambao ni
Mwekezaji wa Shamba la Kapunga(Kapunga Rice Project) lililopo Wilayani
Mbarali Mkoani Mbeya ambao walikuwa wakituhumiwa kwa mashtaka matatu
ambayo ni kula njama, kumwaga sumu na kuharibu mashamba ekari 557 ya
Wananchi.
Akisoma
hukumu Mhakamani hapo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite
alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa
yakiwakabili watuhumiwa ambao ni Waldeman Veemark ambaye ni meneja wa
shamba, Sergei Beacker ambaye ni Afisa Ugani wa kampuni pamoja na rubani
wa ndege Andreas Daffee.
Mteite
alidai kuwa mbali na upande wa mashtaka kuwa na mashahidi 155,ambapo
kati yao mashahidi zaidi ya 20 hawakuweza kufika mahakamani huku wengine
9 wakitoa ushahidi wa uongo tofauti na mashtaka yaliyopelekwa.
Aliongeza
kuwa katika mashahidi hao, Shahidi wa 102 ambaye ni Mtaalam wa Kilimo
wa kijiji cha Kapunga aliyefahamika kwa jina moja la Geophrey alishindwa
kuithibitishia Mahakama utaalamu wa kimaabara kwamba kilichomwagwa na
watuhumiwa hao ni sumu.
Hakimu
huyo alisema pia mashahidi hao zaidi ya 100 hakuna aliyekiri kuwaona
washtakiwa wakitenda kosa hilo licha ya kudai waliiona ndege ikiwa
angani ikinyunyiza vitu vinavyodhaniwa kuwa ni sumu.
Kutokana
na ushahidi huo Hakimu Mteite alisema Mahakama inawaachia huru
washtakiwa wote watatu kwa mujibu wa kifungu cha 312 cha kanuni ya
adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Awali
mwendesha mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa alidai mahakamani hapo
kuwa Watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 12, 2012
kinyume cha sheria namba 336 na kifungu cha 122(i), sura ya 16 kama
ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Ambapo
walidaiwa kuharibu ekari 557.5 za mashamba ya mpunga ya wananchi yenye
thamani ya shilingi zaidi ya Milion 800 kwa kumwaga dawa inayodaiwa kuwa
ni sumu kwenye maji na mazao hali iliyowaathiri kiafya baadhi ya
wananchi.
Kwa
upande wa washtakiwa ambao walikuwa wakitetewa na Wakili Ladislaus
Lwekaza, ambapo wakiwawanajitetea walisema kwamba hawakuhusika na tukio
hilo na kwamba siku ya tukio Meneja alikuwa ofisini ili hali washtakiwa
wengine walidai kuwa hawakuwepo eneo la tukio.
Hata
hivyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite
alimaliza kusoma hukumu hiyo kwa kutoa nafasi kwa upande wa mashtaka
kukata rufaa kwa mujibu wa sheria kutokana na kuwa wazi kama
hawakuridhika na hukumu.
Picha na Ezekiel Kamanga
No comments:
Post a Comment