Wednesday, March 20, 2013

Balozi Seif Ali Idd azindua rasmi safari za ndege za kitalii moja kwa moja kutoka Afrika Kusini hadi Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisoma hotuba ya uzinduzi rasmi wa safari za watalii kutoka moja kwa moja Afrtika kusini hadi Zanzibar kwa usafiri wa shirika la Mango Airlines katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Kisauni Nje kidogo ya mji wa Zanzibar. (Picha na Hassan Issa wa – OMPR-ZNZ).
Rubani wa Ndege ya Shirika la Mango Airlines Kepteni Kevin Viljoen akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar kuanza safari za kuleta abiria kati ya Afrika Kusini na Zanzibar. Nyuma ya Kepteni Kevin ni Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Dunia Haji.
Baadhi ya Watalii 175 waliotua uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa kutumia ndege ya shirika la Mango Airlines wakifurahia ukarimu wa kinywaji cha dafu mara tu baada ya kutua uwanjani hapo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimaliza kuzindua safari za ndege za shirika la Mango Airlines kati ya Afrika Kusini na Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar uliopo Kisauni. Kulia yake ni Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Duni Haji na Kushoto yake ni Mwakilishi wa Shirika la Mango Airlines hapa Zanzibar Bw. Javed Jaffery.

Lowassa afufua kashfa ya kigogo Ikulu

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.
Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.
Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.
Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.
Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.
Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.
“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.
Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.
Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI LEO

Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau akifafanua jambo mbele ya wajumbwe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa daraja la Kingamboni jijini Dar es Salaam leo. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau (wa pili kushoto) akiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi huo leo. Kushoto ni Mhandisi wa NSSF, John Msemwa.
 Mhandisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Msemwa akitoa mada wakati Kamati ya Bunge ya miundombinu ilipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni..
 Naibu Waziri wa
Ujenzi, 
Gerson Lwenge akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi
wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. 
 Kamati ya Bunge ya Miundombinu ikiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
 Mafundi wakiwa kazini.
 Mafundi kazini.
 Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri
wa Ujenzi, 
Gerson Lwenge wakati kamati hiyo
ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Hapa moja ya za daraja la Kigamboni itawekwa hapa.
 Mhandisi wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Karim Mattaka akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi
wa daraja la Kigamboni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Selukamba. 
 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu akiwa na Ofisa wa Trafic, Peter.
 Mhandisi wa NSSF, John Msemwa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa Mkufugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kulia)
 Zege ikimiminwa katika moja ya nguzo za daraja hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter
Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, 
Gerson Lwenge wakati kamati
hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.

KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS YAZINDULIWA RASMI LEO

kili1Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA.kili2Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.kili3
Katikati ni Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL kulia na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kushoto pamoja na Maofisa wa TBL na BASATA wakifurahia jambo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa nembo  ya Kilimanjaro Music Award.
Tuzo za muziki maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam zikiwa na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
George Kavishe, Meneja wa  kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa, “Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini  tuzo hizi kwa mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza washindi.”
Alisema Kilimanjaro Premium  Lager imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na kuwapa tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka  wanamuziki  wetu wajisikie wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya  vile vile tunataka Watanzania  waweze kuthamini muziki wa nyumbani na kutambua mchango wa wanamuziki katika kuleta maendeleo ya uchumi katika nchi.
‘’Kilimanjaro Premium Lager inajivunia  kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu kua mwaka huu tukio hili litakua kubwa na zuri zaidi’’
‘’Pia tuna furaha kutangaza  kwamba BASATA imetupatia leseni ya kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa kipindi cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa Tanzania. Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium Lager kuwa mdhamini wa tuzo hizi mpaka mwaka 2018.

Tuesday, March 19, 2013

MWANAMKE MWENYE WAUME WATANO, AMBAO WOTE NI MAKAKA WA FAMILIA MOJA NA ANALALA NA KILA MMOJA KWA SIKU TOFAUTI

 Huyu ni dada Rajo Verma, mwenye umri wa miaka 21 kaolewa na wanaume watano na cha ajabu zaidi ni kua wanaume hao wote ni ndugu. Rajo anasema kua kutokana na kua na uhusiano na wanaume hao watano imekua ngumu kwake kujua nani ni baba wa mtoto huyo, kwani hulala na wanaume hao wote kwa zamu. Yani leo ni zamu ya huyu na kesho ni zamu ya mwingine.

Wa kwanza kumuoa ni Guddu mwenye umri wa miaka 21, yeye anasema haoni wivu mke wake kulala na kaka zake kwani  ni ndugu zake na wanaishi kwa amani na upendo kama familia moja. Ndugu wengine wa Guddu ni  Bajjumwenye miaka 32, Sant Ram mwenye miaka 28, Gopal mwenye miaka 26, naDinesh ambaye amefikisha miaka 18 mwaka huu.

Rajo anasema kua kipindi anaolewa na mme wake wa kwanza alijua kwamba ni lazima awakubali wanaume hao,kwani hata mama yake Rajo alikua kaolewa na wanaume watatu ndugu wa familia moja

Mwandishi mwingine anusurika kutekwa

Andrew Chale Mwandihi wa Gazeti la Tanzania Daima anayedai kufanyiwa jaribu la kutekwa
Dar es Salaam
MWANDISHI wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima Andrew Chale ameanza kuishi maisha ya wasiwasi baada ya watu wasiojulikana kufanya jaribio la kumteka.
Akizungumza naHabarimpya.comChale alisema kwamba siku ya Jumamosi usiku watu wasiojulikana walikuwa wakifuatilia nyedo zake.
Alisema watu walikuwa kwenye magari mawili yenye rangi na namba za Jeshi la Polisi walikuwa wakimfuta nyuma kila alipokuwa akipita kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.
"Siku ya Jumamosi usiku nikiwa njiai kutoka Kazini, niliona magari mawili ya Polisi yakinifuata kwa karibu na baada ya kuingia uchochoro flani wakuingia nyumbani magari hayo yakapaki"alisema Chale na kuongeza"
"Watu waliokuwa eneo hilo walisema kwamba baada ya magari hayo kupaki wakakaa hapo kwa saa mbili na baadaye walishuka askari watu huku wawili wakivaa nguo za kiraia huku mmoja akiwa na Gazeti la Tanzania Daima mkononi".
Alisema kwamba baada ya watu hao kushuka na kuuliza mtu waliemwita kwa jina la ANDRESON,, ndipo wakaambiwa kwamba hakuna mtu mwenye jina hilo katika mtaa huo lakini , walipoelezea mwonekano wake, wakajibiwa kuwa kijana anayefahamika eneo hilo hupita tu lakini mahali anapoishi hapajulikani.
"Tunayemfahamu ni kijana mmoja ila huwa anapita hapa akiwa na hilo Gazeti majira ya usiku, na wakati mwingine huwa anapita hapa akiwa na mambo yake mengine, baaada ya hapo magari hayo yaliondoka"aliwanukuu mashuhuda wa tukio hilo.
"Watu hao walirudi tena hadi nyuma ya nyumba yangu na nikawasikia wakijitambulisha kuwa wao ni Polisi jamiii na kwamba walikuwa wakimtafuta kijana mmoja ambaye wamesahau anapoishi"alifafanua Chale. SOURCE JAMII FORAM

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA LEOMPIRA WA MIGUU TFF


tff_LOGO1

KIINGILIO MECHI YA STARS, MOROCCO 5,000/-
Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.
 Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000.
 Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.
 Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala.
 Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Vilevile tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo.
 SAMATA, ULIMWENGU WARIPOTI STARS
Washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili nchini jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.
 Ujio wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti kambini leo asubuhi.
 Wachezaji John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri. Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia nayo wenzao kuwa imejaa.

Mtuhumiwa wa uhalifu wa kivita Kongo Jenerali Ntaganda ajisalimisha.


Mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jenerali Bosco Ntaganda, amejisalimisha katika ubalozi wa Marekani mjini Kigali nchini Rwanda.
 Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kuwa Ntaganda aliomba apelekwe katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, iliyoko mjini The Hague, nchini Uholanzi.
Mahakama hiyo ya ICC ilitoa waranti wa kukamatwa kwa Jenerali Ntaganda mwaka 2006.
Lakini mwenyewe amekanusha tuhuma za kuwatumikisha watoto jeshini, kufanya mauaji ya kikabila na ubakaji.
Mashtaka dhidi yake yanahusiana na wakati alipokuwa kiongozi wa wanamgambo kaskazini-mashariki mwa Kongo, kati ya mwaka 2002 na 2003.
Ntaganda pia anaaminika kuwa kiongozi wa kundi la waasi la M23, ambalo linapambana na vikosi vya serikali mashariki mwa nchi hiyo.

IGP SAID MWEMA AIBUKA SAKATA LA DK. ULIMBOKA, KIBANDA.


 IGP SAIDI MWEMA.
 Dk Ulimboka kabla hajaanza kutibiwa.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.




MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema amesema upelelezi wa kesi ya kutekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka bado haujakamilika.

Mbali na Dk. Ulimboka, IGP alisema kesi nyingine zote za aina hiyo pamoja na za mauaji ya watu mbalimbali, akiwemo Padri wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili lililopo Mji Mkongwe Zanzibar, Evaristus Mushi (56), uchunguzi wake unaendelea.
IGP Mwema, aliyasema hayo jana wakati wa semina ya wakuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mjini Dar es Salaam jana.
Dk. Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, alitekwa usiku wa kuamkia Juni 27, 2012. 
Hata hivyo, suala hilo lilizua sintofahamu ya aina yake baada ya mtuhumiwa Joshua Mulundi, raia wa Kenya kukamatwa na kufunguliwa kesi, akishtakiwa kwa kosa la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.
Akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari waliotaka kujua upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi, licha ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kesi hiyo, ambaye anaendelea kusota gerezani, IGP Mwema alisema upelelezi wa kesi unategemea kupatikana mapema kwa ushahidi husika, vinginevyo kesi za aina hiyo zinaweza kuchukua muda mrefu.

Keyshia Cole audiss wimbo mpya wa Beyonce ‘Bow Down’

Ni wiki kadhaa tu zimepita tangu Keyshia Cole amdiss Michelle Williams kwenye performance yake na Destiny’s Child kwenye super bowl na sasa mdomo wake unataka kumuingiza tena matatani kwa kuudiss wimbo mpya wa Beyoncé, Bow Down.
Cole na Bey
“Can’t stand when people all self righteous when it’s convenient it makes them look good. Lmao! But can still talk shit when convenient 2 FOH,” alitweet Keyshia, jana ambaye baadaye aligeuka gumzo kwa kauli hiyo.
Baada ya jana Beyoncé kuachia wimbo huo uliotengenezwa na Hit-Boy, alitweet, “This my shit, bow down, bitches”
Hata hivyo Keyshia aliona wimbo huo kama una kasoro ukizingatia ujumbe wa mwanzo wa Bey kuwa wanawake wanatakiwa kuwa na umoja.
“First ‘Women need to Stick together’ now bitches better Bow. Smh,” aliandika. “But it’s all G! Chicks stay shooting the shit. But when I speak my mind it’s a prob. #Well #StayMad.”
Baada ya mtu mmoja kumtuhumu kwa ana chuki binafsi, Keyshia alijibu, “How am i hating? no Mamm or sir. whatever u may be. No H8.”

Ulinzi mkali sherehe ya Papa

Vatican City. Ulinzi mkali umeandaliwa kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali na wale wa kidini duniani waliowasili jijini Vatican, kwa misa maalumu ya kutawazwa kwa Papa Francis leo.

 
Papa Francis akisalimiana na Rais wa Argentina, Cristina Fernandez de Kirchner alipowasili Vatican, jana kuhudhuria sherehe za kutawazwa kwa mkuu huyo wa Kanisa Katoliki zitakazofanyika leo.
Waumini na wageni milioni moja akiwamo Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk James Msekela, wanatarajiwa kuhudhuria misa hiyo itakayofanyika kwenye Viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Baada ya Papa Francis kutawazwa, ataanza rasmi kazi ngumu ya kuliongoza Kanisa Katoliki lenye waumini wengi na ambalo limekumbwa na mizozo kadhaa ikiwamo ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya makasisi.

Kiongozi huyo alichaguliwa Jumatano iliyopita kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Papa Benedict XVI, aliyejiuzulu Februari 28, mwaka huu.

Misa ya kutawazwa kwa Papa Francis, imeifanya Mamlaka ya Jiji la Rome kuandaa ulinzi mkali kwa watu wote ambao wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.
Tayari, Papa Francis ameduwaza wengi kwa kauli na vitendo vyake vingi ambavyo vinamwonyesha kama kiongozi asiyependa makuu na ambaye pia anatarajiwa kubadili uendeshaji wa kanisa hilo lenye waumini 1.2 bilioni.

Miongoni mwa wageni maalumu waliowasili Italia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Mkatoliki ambaye hii ni mara yake ya pili kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya (EU) dhidi ya utawala wake.

Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo anatarajiwa kuhudhuria. Misa hiyo imewekwa rasmi kwa kumbukumbu ya Mtakatifu Yosefu, ambaye ndiye msimamizi wa kiimani wa Taifa la Italia, mahali iliko Vatican.

Wengine ni Rais wa Argentina, Cristina Kirchner na mpinzani wa Papa Francis ambaye jana alitarajiwa kukutana naye kwa mazungumzo ya faragha. Wawili hao wamekuwa wakisigana katika masuala mengine yakiwamo ndoa za mashoga na utoaji mimba.

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff amewasili pia kama ilivyo kwa mwenzake wa Mexico, Enrique Pena Nieto. Pia, Rais wa Chile, Sebastian Pinera aliwasili Rome tangu Jumapili kwa misa ya kwanza ya Papa Francis. Rais huyo ni miongoni mwa wageni maarufu. Yumo pia Makamu wa Rais wa Ufilipino, Jejomar Binay akimwakilisha Rais Benigno Aquino III.

Orodha hiyo inawajumuisha pia Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Waziri Mkuu wa Hispania, Mariano Rajoy , Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault , Rais wa EU, Herman Van Rompuy, Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barroso.

Wengine ni mwakilishi wa Kanisa la Anglikana, Askofu Mkuu wa York, John Sentamu. Pia, Ibrahim Isaac Sidrak, kutoka Jumuiya ya Wakoptiki ya Kanisa Katoliki, Alexandria, Misri na Metropolitan Hilarion, ambaye ni mkuu msaidizi wa Kanisa la Orthodox , Russia.
*Ndyesumbilai Florian kwa msaada wa mtandao

SAKATA LA TUNDU LISSU KUJIFUNGIA CHOONI

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

ZIPO taarifa kwamba Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, wiki iliyopita alijifungia chooni kukwepa waandishi wa habari waliotaka kauli yake juu ya video hatari ambayo inadaiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Rwakatare, alirekodiwa akieleza njama za uhalifu.
Tundu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amesema kuwa maelezo yaliyotolewa kwamba alijificha chooni kwa muda wa saa mbili si kweli, kwani hawezi kufanya hivyo.
“Jamani mimi na umri wangu huu nawezaje kuwakimbia waandishi wa habari? Siku zote mimi nafanya kazi na waandishi wa habari,” alisema Lissu na kuongeza:
“Ofisi yangu pale Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam ina choo ndani, nikiwa ofisini kama mtu yupo nje wala hawezi kujua kama mimi nipo chooni. Nadhani hizo taarifa za kusema nilijifungia chooni ni za upotoshaji.

“Halafu haiwezekani mimi nikimbie suala la Rwakatare kwa sababu tayari nilishalitolea maelezo. Mpaka sasa, mimi kama mmoja wa mawakili wanaomtetea, nina maswali yangu kwa jeshi la polisi, kwani ile video haioneshi uhalifu wowote ambao umetendeka.
“Ni kweli niliweka miadi ya kuzungumza na waandishi lakini nilisahau. Nakumbuka jioni kabisa ya siku hiyo, nilipokea SMS ya mwandishi, akiniambia alikaa sana Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam mpaka akachoka, kwa hiyo alishindwa kuniona.”
Wikiendi iliyopita, iliripotiwa na mitandao mbalimbali pamoja na gazeti moja la kila siku kwamba Lissu alijificha chooni kwa saa mbili kukwepa kuonana na waandishi wa habari, waliotaka ufafanuzi wake kuhusu kile kinachoendelea juu ya kesi inayomkabili Rwakatare ambaye ni Kiongozi Mstaafu wa Kambi ya Upinzani Bungeni. 
SOURCE GLOBAL PUBLISHER

Tigo yakabidhiwa Tuzo kwa kuwawekea wananchi huduma ya SMS itakayowawezesha kujua hali ya FIGO zao popote walipo.

 

Waziri mkuu Mh.Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya shukrani kwa Mkurugenzi wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez kwa ajili ya mchango wao katika kuwaletea wananchi huduma ya sms ambayo itawawezesha wananchi kujua hali za figo zao popote walipo kupitia simu zao za mkononi.

MTOTO WA RAIS KUSHITAKIWA ARUSHA.

 
Kwa ufupi
Saif al-Islam Gaddafi, ambaye ni mtoto wa pili wa Gadaffi amekuwa akishikiliwa na vyombo vya usalama vya Libya tangu Novemba 19, 2011 baada ya kukamatwa wakati akijaribu kukimbia nchi hiyo baada ya kuuawa kwa baba yake na kaka yake, Mtassim Gaddafi,

Mahakama ya Afrika inayoshughulikia haki za binadamu yenye makao yake jijini Arusha imeamuru  Serikali ya Libya kuendesha kesi inayomkabili mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gadaffi kwa uhuru na haki.
Saif al-Islam Gaddafi, ambaye ni mtoto wa pili wa Gadaffi amekuwa akishikiliwa na vyombo vya usalama vya Libya tangu Novemba 19, 2011 baada ya kukamatwa wakati akijaribu kukimbia nchi hiyo baada ya kuuawa kwa baba yake na kaka yake, Mtassim Gaddafi, Oktoba 20, 2011.
Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika yenye makao makuu mjini Addis Ababa, Ethiopia ndiyo iliyowasilisha shauri hilo kwenye Mahakama ya Afrika kwa kuwa Serikali ya Libya haijaridhia mikataba ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Kutokana na hali hiyo, hata familia ya Gadaffi ilishindwa kufungua kesi hiyo kwani taasisi au watu binafsi wa Libya hawana uwezo wa kisheria wa kufungua kesi kwenye mahakama hiyo kutokana na kikwazo cha Serikali yao.
Shauri hilo lenye namba 002/2012 lilisikilizwa na majaji kumi na moja walioongozwa na Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Sophia Akuffo kutoka Ghana, Ijumaa iliyopita.
Wengine waliokuwemo kwenye jopo hilo ni pamoja na Makamu wake, Jaji Fatsah Ouguergouz, Jaji Mkuu wa zamani, Augustine Ramadhan pamoja na Majaji Sylvain Ore, Duncan Tambala, Gerald Niyugeko, Bernard Ngoepe, Elsie Thompson, Hadji Guisse, Kimelabalou Aba na Ben Kioko.
Jopo hilo la majaji pia limeiamuru Serikali ya Libya kuruhusu ndugu, jamaa na marafiki wa mtuhumiwa huyo kumtembelea kipindi chote shauri dhidi yake linaposikilizwa.
Serikali ya Libya imetakiwa kutoa taarifa mahakamani kuhusu utekelezaji wa amri hiyo siku 15 tangu kupokelewa kwa nakala ya hukumu.
Familia ya Gadaffi imekuwa haifurahishwi na mwenendo wa kesi ya  Saif huko Libya.

MUGABE ATINGA VATICAN KUHUDHURIA KUTAWAZWA KWA PAPA FRANSIS I

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili nchini Italia jana kwa ajili ya kuhudhuria kutawazwa  kwa Papa Francis na maafisa wamejaribu kupuuzia ukiukaji wa kiutaalamu wa marufuku ya kusafiri  katika mataifa ya Umoja wa Ulaya dhidi ya kiongozi huyo wa siku nyingi barani Afrika.

Mugabe, ambaye amepigwa marufuku kuingia katika mataifa ya Ulaya tangu mwaka 2002 kwa sababu ya  madai ya udanganyifu katika kura na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe, alichukuliwa  moja kwa moja kutoka katika ndege iliyomleta mjini Rome kwa gari, pamoja na mkewe, Grace na  walinzi wake. 

Licha ya kuwa uwanja huo wa ndege uko katika ardhi ya Italia, kiongozi huyo mwenye  umri wa miaka 89 alilakiwa na padri, ambaye alimwambia: "Kwa niaba ya Papa Francis, karibu  Vatican, karibu mahali patakatifu". Baadaye alipelekwa katika hoteli katika eneo maarufu la Via Veneto. Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, anatawazwa rasmi leo Jumanne.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...