Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo
za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa
Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA.Kushilla
Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey
Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba
huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.
Katikati ni Kushilla
Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL kulia na Godfrey Mngereza Kaimu
Katibu Mtendaji wa BASATA kushoto pamoja na Maofisa wa TBL na
BASATA wakifurahia jambo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa nembo ya
Kilimanjaro Music Award.
Tuzo za muziki maarufu kama Kilimanjaro
Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam zikiwa
na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta
ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
George Kavishe, Meneja wa kinywaji cha
Kilimanjaro Premium Lager amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa,
“Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa
mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa
kuwapata wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8
Juni ambapo tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza
washindi.”
Alisema Kilimanjaro Premium Lager
imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na kuwapa
tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka wanamuziki wetu wajisikie
wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya vile vile
tunataka Watanzania waweze kuthamini muziki wa nyumbani na kutambua
mchango wa wanamuziki katika kuleta maendeleo ya uchumi katika nchi.
‘’Kilimanjaro Premium Lager inajivunia
kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu kua mwaka huu tukio hili
litakua kubwa na zuri zaidi’’
‘’Pia tuna furaha kutangaza kwamba
BASATA imetupatia leseni ya kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa kipindi
cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni
uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa
Tanzania. Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium Lager kuwa mdhamini
wa tuzo hizi mpaka mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment