Wapiga kura nchini Zimbabwe wameunga mkono
mabadiliko ya katiba.
Katika kura ya maoni iliyopigwa mwishoni
mwa wiki ililopita, asilimia 95 ya wapiga kura hao wamepiga kura ya
ndio.
Kura hiyo imetayarisha mchakato wa uchaguzi
mwishoni mwa mwaka huu, ambao utamaliza kipindi cha utawala wa mpito
wenye mivutano, unaoshirikisha rais Robert Mugabe na mpinzani wake
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai.
Mabadiliko hayo ya katiba yanaweka kikomo
cha mihula miwili ya miaka mitano kwa rais, na yanalipa bunge madaraka
makubwa.
Mabadiliko hayo hali kadhalika yanaondoa
wadhifa wa Waziri Mkuu.-DW.
No comments:
Post a Comment