IGP SAIDI MWEMA.
Dk Ulimboka kabla hajaanza kutibiwa.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
MKUU
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema amesema upelelezi wa kesi
ya kutekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka bado haujakamilika.
Mbali
na Dk. Ulimboka, IGP alisema kesi nyingine zote za aina hiyo pamoja na
za mauaji ya watu mbalimbali, akiwemo Padri wa Kanisa Katoliki la Minara
Miwili lililopo Mji Mkongwe Zanzibar, Evaristus Mushi (56), uchunguzi
wake unaendelea.
IGP
Mwema, aliyasema hayo jana wakati wa semina ya wakuu wa Upelelezi wa
makosa ya Jinai wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC), Mjini Dar es Salaam jana.
Dk. Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, alitekwa usiku wa kuamkia Juni 27, 2012.
Hata
hivyo, suala hilo lilizua sintofahamu ya aina yake baada ya mtuhumiwa
Joshua Mulundi, raia wa Kenya kukamatwa na kufunguliwa kesi, akishtakiwa
kwa kosa la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.
Akijibu
maswali mbalimbali ya waandishi wa habari waliotaka kujua upelelezi wa
kesi hiyo umefikia wapi, licha ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kesi hiyo,
ambaye anaendelea kusota gerezani, IGP Mwema alisema upelelezi wa kesi
unategemea kupatikana mapema kwa ushahidi husika, vinginevyo kesi za
aina hiyo zinaweza kuchukua muda mrefu.
No comments:
Post a Comment