Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili
nchini Italia jana kwa ajili ya kuhudhuria kutawazwa kwa Papa Francis na
maafisa wamejaribu kupuuzia ukiukaji wa kiutaalamu wa marufuku ya
kusafiri katika mataifa ya Umoja wa Ulaya dhidi ya kiongozi huyo wa siku
nyingi barani Afrika.
Mugabe,
ambaye amepigwa marufuku kuingia katika mataifa ya Ulaya tangu mwaka 2002 kwa
sababu ya madai ya udanganyifu katika kura na ukiukaji wa haki za
binadamu nchini Zimbabwe, alichukuliwa moja kwa moja kutoka katika ndege
iliyomleta mjini Rome kwa gari, pamoja na mkewe, Grace na walinzi wake.
Licha
ya kuwa uwanja huo wa ndege uko katika ardhi ya Italia, kiongozi huyo
mwenye umri wa miaka 89 alilakiwa na padri, ambaye alimwambia: "Kwa
niaba ya Papa Francis, karibu Vatican, karibu mahali patakatifu".
Baadaye alipelekwa katika hoteli katika eneo maarufu la Via Veneto. Kiongozi wa
Kanisa Katoliki, Papa Francis, anatawazwa rasmi leo Jumanne.
No comments:
Post a Comment