Baada
ya mazungumzo pamoja na viongozi wa serikali ya nchi hiyo , Rais Gauck
aliwahutubia wawakilishi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.
Hotuba
ya Rais Gauck mbele ya wawakilishi wa Umoja wa Afrika ilikuwa ikiangaliwa kama
kilele cha ziara ya siku nne ya rais huyo wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
nchini Ethiopia. Rais Gauck alizungumzia zaidi kuhusu
demokrasia na haki za binaadamu.
Mwanasiasa
huyo mwenye umri wa miaka 73 amewatolea mwito viongozi wa Afrika wafungue
ukurasa mpya wa demokrasia na utawala unaofuata sheria. Rais Gauck amesema
kuwa "Afrika inabidi izishinde changamoto zilizoko na kubuni
njia ya Kiafrika kuelekea demokrasia".
Rais
Gauck amezitaka nchi zote za Afrika ziwe na serikali
zilizochaguliwa kwa njia za kidemokrasia na bunge kujipatia madaraka makubwa
zaidi.
No comments:
Post a Comment