Dar es Salaam
MWANDISHI
wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima Andrew Chale ameanza kuishi
maisha ya wasiwasi baada ya watu wasiojulikana kufanya jaribio la
kumteka.
Akizungumza naHabarimpya.comChale alisema kwamba siku ya Jumamosi usiku watu wasiojulikana walikuwa wakifuatilia nyedo zake.
Alisema
watu walikuwa kwenye magari mawili yenye rangi na namba za Jeshi la
Polisi walikuwa wakimfuta nyuma kila alipokuwa akipita kuelekea nyumbani
kwake maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.
"Siku
ya Jumamosi usiku nikiwa njiai kutoka Kazini, niliona magari mawili ya
Polisi yakinifuata kwa karibu na baada ya kuingia uchochoro flani
wakuingia nyumbani magari hayo yakapaki"alisema Chale na kuongeza"
"Watu
waliokuwa eneo hilo walisema kwamba baada ya magari hayo kupaki wakakaa
hapo kwa saa mbili na baadaye walishuka askari watu huku wawili wakivaa
nguo za kiraia huku mmoja akiwa na Gazeti la Tanzania Daima mkononi".
Alisema
kwamba baada ya watu hao kushuka na kuuliza mtu waliemwita kwa jina la
ANDRESON,, ndipo wakaambiwa kwamba hakuna mtu mwenye jina hilo katika
mtaa huo lakini , walipoelezea mwonekano wake, wakajibiwa kuwa kijana
anayefahamika eneo hilo hupita tu lakini mahali anapoishi hapajulikani.
"Tunayemfahamu
ni kijana mmoja ila huwa anapita hapa akiwa na hilo Gazeti majira ya
usiku, na wakati mwingine huwa anapita hapa akiwa na mambo yake mengine,
baaada ya hapo magari hayo yaliondoka"aliwanukuu mashuhuda wa tukio
hilo.
"Watu
hao walirudi tena hadi nyuma ya nyumba yangu na nikawasikia
wakijitambulisha kuwa wao ni Polisi jamiii na kwamba walikuwa
wakimtafuta kijana mmoja ambaye wamesahau anapoishi"alifafanua Chale.
SOURCE JAMII FORAM