Monday, March 11, 2013

FIFA yaichimba mkwara Serikali ya Bongo


Taarifa zilizoingia hivi punde ni kwamba shirikisho la kimataifa la soka duniani FIFA limeifungia Tanzania kwenye mashindano yote ya kimataifa yaliyo chini. Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mtandao huu.
source shaffih dauda

Duuuuh!! mtoto wa miaka 8 afunga ndoa na bibi yake

Eight-Year Old Sanele Masilela walks down the aisle with his 
61-year-old bride Helen Shabangu at their wedding ceremony in Tshwane, 
South Africa
Eight-Year Old Sanele Masilela walks down the aisle with his 61-year-old bride Helen Shabangu at their wedding ceremony in Tshwane, South Africa
Ceremony: The schoolboy kisses his 61-year-old bride, who is 
already married and a mother of five. He said he had been told to tie 
the knot by his ancestors
With this ring: The boy's family say the wedding was simply a 
ritual and not recognised in law
With this ring: The boy's family say the wedding was simply a ritual and not recognised in law


Duniani kuna mambo --- Dogo wa miaka 8 aliyeoa mwanamke wa miaka 61 nchini Afrika Kusini.

WANANCHI WA MOROGORO WAMPONGEZA PADRE RICARDOMARIA

Padre Ricardo Maria ambaye anamiliki shule mbili za sekondari mkoani morogoro nilimnasa juzi kati pande za Mji mpya mkoani hapa akielekea kwenye moja wa shule zake zilipo maeneoe ya Nane Nane akitumia usafiri wake wa baiskeli.

Habari kutoka ndani ya shule hizo za raia huyo wa ltalia zinadai kwamba mtumishi huyo wa mungu asiye vaa viatu kutokana na imani ya dhehebu lake,hupokea watoto yatima na kuwasomesha bure kwenye shule zake. 

Mungu akubariki sana mtumishi wa mungu usiyekuwa na makuu licha ya kujaliwa kuwa na kipato kizuri ikumbukwe pia Padre huyu ni mmoja wa wakurugenzi wa Radio Ukweli inayomilikiwa na kanisa katoriki jimbo la Morogoro.[PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO]

Tigo yampeleka nchini China Mshindi wa Promosheni ya Ascend Y200 Bw.Christian Mkama.


Mshindi wa droo ya Ascend Y200 ya mwaka jana bw. Christian Evarist Mkama akiongea na waandishi wa habari uwanja wa ndege wa kimataifa JK Nyerere kabla ya safari kuelekea nchini China.
Mshindi wa droo ya Ascend Y200 ya mwaka jana bw. Christian Evarist Mkama akiwa na mama mzazi Bi. Eva Christian Amuko na mjomba wake bw. Fortunatus Christian Amuko uwanja wa ndege JK Nyerere kabla ya safari kuelekea nchini China.
Tigo Tanzania imempeleka Bw. Christian Evarist Mkama nchini China ambaye ni mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya kwanza ya Ascend Y200 ambayo ilifanyika mwaka jana tarehe 19 Desemba.
 
Kwa kuwa mshindi wa droo hii amejishindia tiketi ya bure ya kwenda na kurudi nchini China pamoja na kulipiwa gharama zote za safari,chakula na dola 200 kwa siku za matumizi.
 
Akiwa nchini china mshindi huyu atakaa siku nne na atatembezwa na kuonyeshwa sehemu mbalimbali za mji wa Guangzhou, na kupelekwa kwenye sehemu za utalii ya mlima Lotus.
 
Promosheni ya AscendY200 ilizinduliwa mwaka jana 2012 mwezi wa kumi(oktoba) kwa jumla kutakuwa na droo tano za Ascend Y200 na kila droo itakuwa na washindi wawili kwa jumla ya washindi kumi watapatikana kwenye droo hizi.
 
Kushiriki kwenye shindano hili mteja wa Tigo inambidi awe amenunua simu ya Ascend Y200 kwenye maduka ya Tigo yaliyosajiliwa na kujisajili kwenye kifurushi cha A-Smart package.

GHASIA ZAIBUKA KENYA




Polisi wa kutuliza ghasia, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi nchini Kenya, mji wa Kisumu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya urais ambayo mgombea wao, Raila Odinga alishindwa katika uchaguzi uliofanyika nchini humo.
Vurugu hizo ziliibuka, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.

DOKEZO
Mahakama Kuu ya Kenya ndicho chombo pekee chenye uwezo wa kutengua matokeo ya urais yaliyotangazwa IEBC.

Jopo la majaji watano ndilo litakalosikiliza rufaa ya mgombea wa Cord, Raila Odinga; nao ni Jaji Mkuu, Dk. Willy Mutunga ambaye ni Rais wa Mahakama hiyo, wengine ni Majaji Dk. Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Philip Tunoi, Jackton Boma Ojwang na Mohamed Ibrahim.

Source: Mwananchi, Jumatatu, Marchi 11, 2013

MAAFISA WA POLISI MBEYA WASIMAMISHWA KAZI KWA UPOTEVU WA DAWA ZA KULEVYA

Sehemu ya mbele ya gari ikiwa imefunguliwa kwa uchunguzi zaidi
Picha chini :Askari polisi akilinda sehemu ya madawa ya kulevya yaliyotolewa kwenye gari hiyo

TAARIFA zilizotufikia hivi punde zimesema kuwa Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi amewasimamisha kazi badhi ya maofisa wa polisi kwa upotevu wa madawa ya kulevya uliotokea mwaka jana 2012 mkoani Mbeya katika mazingira ya kutatanisha.

Baadhi ya maofisa hao ni kamanda wa kikosi cha upelelezi mkoani Mbeya (RCO) Elis Mwita, naibu RCO Jacob Kiangi na mkuu wa kikosi cha FFU Charles Kinyongo.

WAKATI WABUNGE WAKITESA, MADEREVA WAO WALIA NA NJAA KALI

WAKATI wananchi wengi, wakikabiliwa na ugumu wa maisha, madereva wa wabunge nao wameibua kilio chao wakilalamikia ukali wa maisha. Madereva hao, walilazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila wakilalamikia haki zao kukaliwa na wabunge. MTANZANIA imefanikiwa kunasa barua hiyo ya Julai, 2012 ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Wabunge, Juvenille Joseph.

Pamoja na mambo mengine, barua hiyo inaishutumu Ofisi ya Bunge kushindwa kusimamia maslahi yao, hali inayowafanya waishi kwa shida.

Katika barua hiyo, madereva hao walilamikia suala la ukosefu wa mikataba ya kazi, huku wakitaka posho na mishahara yao itenganishwe kutoka katika akaunti za wabunge.

“Mheshimiwa Katibu wa Bunge, sisi ni madereva wa waheshimiwa wabunge, tunaleta kwako hoja zetu ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kina katika ofisi yako.

“Kwa kipindi chote, madereva wa wabunge hatukuwa na mikataba ya ajira zaidi ya makubaliano ya mdomo baina ya dereva na mbunge.

“Ndiyo maana kunakuwa na unyanyasaji mkubwa kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge dhidi ya madereva wao.


“Tunaomba ofisi yako izingatie kuwa kazi ya ubunge ni ya kipindi cha miaka mitano, bila mkataba ni vigumu kujua suala la haki za kikazi.

“Hivyo basi, tunaomba ofisi yako isimamie kuhakikisha kuwa wabunge wote wanatoa mikataba ya ajira kwa madereva wao,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

WALIOSEMA MHE. LOWASSA ALIKUWA HAPENDWI NA MWALIMU NYERERE NA AELEWANI NA FAMILIA YAKE WAUMBUKA

Ni baada ya kualikwa kuongoza harambee ya kuchangia miradi ya maendeleo Wilayani Butiama



Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakiwasili kwenye hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick Mugoya.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache kabla ya kuanza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya usimamizi wa Padri Wojciech Adam (hayupo pichani) wa kanisa Katoliki la Kiabakari lililopo wilayani humo,Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere akizungumza machache wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.ambapo Mgeni Rasmi katika harambee hiyo,alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari akitoa historia fupi ya mradi huo toka kuanza kwake mpaka walipofikia wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.ambapo Mgeni Rasmi katika harambee hiyo,alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akizungumza machache wakati wa kukabidhi mchango wake na kuahidi kuendelea kuchangia ili kuhakikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara inafanikiwa huku akisikilizwa kwa makini na Mgeni Rasmi wa Harambee hiyo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono akikabidhi mchango wake kwa Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere huku akisaidiwa na Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkaribisha Brigedia Jenerali,Zoma Kongo kukabidhi mchango wake kwa Mama Maria Nyerere kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.
Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media,Ansbert Ngurumo ampa mkono Mama Maria Nyerere mara baada ya kutoa ahadi yake ya kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkabidhi picha Boss Mkuu wa Mgahawa wa BreakPoint mara baada ya kununua kwenye mnada aliouendesha yeye mwenyewe.Katikati ni Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere.
Padri Wojciech Adam wa kanisa Katoliki la Kiabakari akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mh. Nimrod Mkono.
Rais wa Bodi ya Mradi huo,Dkt. Patrick Mugoya akizungumza machache kwenye hafla hiyo.
Meza kuu.
Mke wa Baba wa Taifa,Mama Maria Nyerere (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) wakiwa kwenye hafla ya kuchangisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Butiama mkoa wa Mara chini ya Padri Wojciech Adam (katikati) wa kanisa Katoliki la Kiabakari,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
 
 
Wadau Mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo.
NA ISSA MICHUZI MATUKIO

Sunday, March 10, 2013

Waziri Acharukia Skendo ya Jack Chuzi Kujiuza

BAADA ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anadaiwa kuicharukia skendo hiyo ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu.


Chanzo cha habari kutoka ndani ya shirikisho hilo kililitonya Ijumaa kuwa, Mhe. Makalla alimvaa Mwakifwamba kwenye mkutano na wasanii uliofanyika ndani ya Hoteli ya Kibadamu, Ubungo jijini Dar.
“Mhe. Makalla ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, akiwa pale alimuuliza Mwakifwamba kuhusu hatua walizochukua kwa Jack Chuzi baada ya kuandikwa habari kuwa alinaswa akienda kuuzwa.


“Mwakifwamba alijitetea kuwa, wanalishugulikia na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ akasisitiza kuwa, wako katika mchakato wa kulitolea uamuzi tukio hilo lililofanywa na Jack ,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi paparazi wetu alimtafuta Mwakifwamba lakini hakuweza kupatikana mara moja ila Mike alipoulizwa juu taarifa za Mhe. Makalla kucharukia ishu ya Jack alisema:

“Ni kweli waziri aliuliza kuhusu hatua tulizozichukua kuhusu suala la Jack kujiuza ambapo nilimjibu kuwa tuko kwenye mchakato wa kulitolea uamuzi na kwa sasa tumeunda kamati maalum, ikimaliza uchunguzi wake ndiyo tutatoa jibu kuwa tumemchukulia hatua gani.”

Source:Global Publisher

MZEE MANDELA APELEKWA TENA HOSPITALINI AFRIKA YA KUSINI.


Former South African President Nelson Mandela 
RAIS Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekea hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Taarifa kutoka kwa afisa ya Rais wa Afrika Kusini zimesema kuwa uchunguzi huu ni wa kawaida tu.

Kwa muujibu wa tovuti ya Urais wa Afrika Kusini, Madaktari wanaomfanyia uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya kuwa na tahariku.

Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni swala la kutia wasiwasi.

Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi wa Desemba mwaka jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja vijiwe ndani ya kibofu chake cha mikojo.

Taarifa iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma zimeeleza kuwa Mzee Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa uchunguzi wa kawaida wa ki-afya.

Taarifa hiyo imeendelea kusima kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutikana na matatizo yanayoambatana na Umri wake mpevu.

Mzee Mandela alifudumu kama rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 to 1999 na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi hiyo.

Kutokana na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za ubaguzi wa rangi nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama Baba wa Taifa nchini Afrika Kusini.

Tangu mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au kushiriki katika shughuli za umma.

BASI LA KILIMANJARO LAPATA AJALI LEO


.
..
Picha na ripoti zimetoka kwa mwandishi michuzijr.blogspot.com

Kamati ya Utendaji CHADEMA Wilaya ya Tarime yavunjwa




Baada ya kikao cha ndani kati ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani, kubaini udhaifu wa kiuongozi ulioruhusu kuzuka kwa makundi yaliyokuwa yakidhoofisha utendaji kazi na uhai wa chama wilayani hapa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amevunja uongozi wa wilaya hiyo (kwa maana ya Kamati ya Utendaji).

Uamuzi huo uliofanyika leo mchana, ulipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wa kikao hicho.


Baada ya kikao hicho cha Kamati ya Utendaji na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Mwenyekiti Mbowe alikutana na wanachama na wadau wa chama wa Tarime, kwenye kikao cha ndani, ambapo kwa kauli moja waliupokea kwa furaha uamuzi huo wa kuvunjwa kwa uongozi huo, huku wakiomba nafasi hizo za uongozi zijazwe mapema kwa ajili ya kuendelea kukiimarisha chama.


Uongozi wa chama katika ngazi za kata hadi misingi utaendelea kufanya kazi kama kawaida.


Kwa hatua hiyo, uchaguzi wa kupata uongozi wa Kamati ya Utendaji ya muda, utafanyika ndani ya mwezi mmoja ukisimamiwa na ngazi ya juu


Mwenyekiti Mbowe amewataka watu wa Tarime kutopoteza ari yao ya dhati katika kukisimamia na kukipigania CHADEMA katika kuendesha mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi, ambayo ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa wanaChadema nchi nzima, kiasi cha watu kusalimiana..."mambo...kama Tarime..."

MAMA PINDA AHIMIZA AKINAMAMA KUWA WAZI NA WAAMINIFU


MKE wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda amewataka akinamama wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali kuwa waaminifu kwa wenza wao na wanafamilia wao ili waweze kupata ushirikiano kutoka kwao.

Alisema mbali ya majukumu mengi yanayowakabili, akinamama wanapaswa kuwa karibu na familia zao kwani ndiyo msingi mkuu wa Taifa. “Hatuna budi kutoa malezi mema kwa wenza wetu na watoto wetu. Tunapofanikiwa katika shughuli zetu, tusiache kuwa waaminifu kwa wana-familia wetu (akinababa na watoto wetu); tuwaheshimu na kuwaenzi kwa kuwashirikisha kazi tunazofanya ili tuweze kupata ushirikiano wao na baraka zao,” alisema.
Mama Pinda ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumamosi, Machi 10, 2013) wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali walioshiriki Maonyesho Maalum ya Batik (Batik Gala Night) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwenye ukumbi wa Hellenic Club, Upanga jijini Dar es Salaam.

Maonyesho hayo yaliandaliwa na Kamati ya Tamasha la Wanawake Wajasiriamali Tanzania (MOWE) kwa kushirikiana na Ofisi ya Shirika la Kazi Duniani hapa nchini (ILO) yalikuwa na nia ya kuamsha chachu ya kuendeleza kazi za akinamama wanaofanya maonyesho kila mwaka yaliyopangwa kufanyika Oktoba, mwaka huu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Alisema akinamama wanapaswa kuungana kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze kuunganisha ujuzi, stadi walizonazo na kushirikishana uzoefu. Alisema hawana budi kuhakikisha kuwa bidhaa wanazozalisha zinakuwa na ubora wa kiwango cha juu ili waweze kukabiliana na ushindani kwenye soko.
 
“Napenda kusisitiza, suala la ubora wa bidhaa tunazozizalisha kwa kuzingatia viwango vya Kitaifa na kimataifa ili bidhaa zetu ziweze kupata uhakika wa soko. Hili litafanikiwa pia endapo tutazingatia pia ubora wa vifungashio tunavyotumia kwenye bidhaa zetu. Endapo, tutazingatia viwango, vifungashio na kutumia kiandishi-anuani (barcodes), sioni ni kwa nini bidhaa zetu zisiende hadi masoko ya mbali huko ughaibuni,” alisema.
 
Aliwataka akinamama wajipange vizuri kwa ajili ya Maonyesho makubwa ya kitaifa (MOWE) yatakayofanyika Oktoba mwaka huu ambayo yatajumuisha washiriki kutoka mikoa yote hapa nchini.

 Mapema, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi hapa nchini (ILO Tanzania), Bw. Alexio Musindo, alisema anawapongeza akinamama wajasiriamali chini ya kamati ya MOWE kwani kupitia mafunzo yanayodhaminiwa na Ofisi yake, akianamama hao wameweza kujiamini zaidi na kuthubutu kushiriki maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Alisema jamii haina budi kuwekeza zaidi kwa wasichana kwa kuwapa fursa za kujiendesha kibiashara pamoja na ujuzi (skills) ili waweze kujiajiri kwani wanakumbana na vikwazo vingi wanapotafuta ajira ikiwemo, unyanyasaji na unyanyapaa.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 3021,

DAR ES SALAAM.

Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania





1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.

-- 

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

Rais Kikwete amtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi nyingi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.
Katika salamu hizo zilizotumwa leo, Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta:
“Mpendwa Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu, kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu binafsi kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya kuchaguliwa kwako.”
Ameongeza Rais Kikwete: “ Ushindi huu ni ushahidi na ishara ya wazi kabisa ya imani na matumaini ambayo wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni utambuzi wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa ambao umeutoa katika nafasi mbali mbali za uongozi katika siku za nyuma katika jitihada zako za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na wananchi wake.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda kukuhakikishia msimamo wangu binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu wa  kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa kwamba pamoja tutaweza kuendelea kusukuma mbele zaidi maendeleo ya nchi zetu – Kenya na Tanzania na pia utengamano wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wake.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
9 Machi, 2013

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...