BAADA
ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’
kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anadaiwa kuicharukia skendo hiyo
ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon
Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya
shirikisho hilo kililitonya Ijumaa kuwa, Mhe. Makalla alimvaa
Mwakifwamba kwenye mkutano na wasanii uliofanyika ndani ya Hoteli ya
Kibadamu, Ubungo jijini Dar.
“Mhe. Makalla ndiye aliyekuwa
mgeni rasmi, akiwa pale alimuuliza Mwakifwamba kuhusu hatua walizochukua
kwa Jack Chuzi baada ya kuandikwa habari kuwa alinaswa akienda kuuzwa.
“Mwakifwamba alijitetea kuwa,
wanalishugulikia na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Michael
Sangu ‘Mike’ akasisitiza kuwa, wako katika mchakato wa kulitolea uamuzi
tukio hilo lililofanywa na Jack ,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi
paparazi wetu alimtafuta Mwakifwamba lakini hakuweza kupatikana mara
moja ila Mike alipoulizwa juu taarifa za Mhe. Makalla kucharukia ishu ya
Jack alisema:
“Ni kweli waziri aliuliza kuhusu
hatua tulizozichukua kuhusu suala la Jack kujiuza ambapo nilimjibu kuwa
tuko kwenye mchakato wa kulitolea uamuzi na kwa sasa tumeunda kamati
maalum, ikimaliza uchunguzi wake ndiyo tutatoa jibu kuwa tumemchukulia
hatua gani.”
Source:Global Publisher
No comments:
Post a Comment