Polisi wa
kutuliza ghasia, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi nchini Kenya,
mji wa Kisumu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya
urais ambayo mgombea wao, Raila Odinga alishindwa katika uchaguzi
uliofanyika nchini humo.
Vurugu hizo ziliibuka, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais
yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.
DOKEZO
Mahakama Kuu ya Kenya ndicho chombo pekee chenye uwezo wa kutengua
matokeo ya urais yaliyotangazwa IEBC.
Jopo la
majaji watano ndilo litakalosikiliza rufaa ya mgombea wa Cord, Raila
Odinga; nao ni Jaji Mkuu, Dk. Willy Mutunga ambaye ni Rais wa Mahakama
hiyo, wengine ni Majaji Dk. Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Philip Tunoi,
Jackton Boma Ojwang na Mohamed Ibrahim.
Source: Mwananchi,
Jumatatu, Marchi 11, 2013
No comments:
Post a Comment