WAKATI wananchi wengi,
wakikabiliwa na ugumu wa maisha, madereva wa wabunge nao wameibua kilio
chao
wakilalamikia ukali wa maisha. Madereva hao, walilazimika kumwandikia
barua
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila wakilalamikia haki zao kukaliwa na
wabunge. MTANZANIA imefanikiwa kunasa barua hiyo ya Julai, 2012 ambayo
imesainiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Wabunge, Juvenille
Joseph.
Pamoja
na mambo mengine,
barua hiyo inaishutumu Ofisi ya Bunge kushindwa kusimamia maslahi yao,
hali
inayowafanya waishi kwa shida.
Katika
barua hiyo,
madereva hao walilamikia suala la ukosefu wa mikataba ya kazi, huku
wakitaka
posho na mishahara yao itenganishwe kutoka katika akaunti za
wabunge.
“Mheshimiwa
Katibu wa
Bunge, sisi ni madereva wa waheshimiwa wabunge, tunaleta kwako hoja zetu
ili
ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kina katika ofisi yako.
“Kwa
kipindi chote,
madereva wa wabunge hatukuwa na mikataba ya ajira zaidi ya makubaliano
ya mdomo
baina ya dereva na mbunge.
“Ndiyo
maana kunakuwa na unyanyasaji mkubwa kwa
baadhi ya waheshimiwa wabunge dhidi ya madereva wao.
“Tunaomba
ofisi yako
izingatie kuwa kazi ya ubunge ni ya kipindi cha miaka mitano, bila
mkataba ni
vigumu kujua suala la haki za kikazi.
“Hivyo
basi, tunaomba
ofisi yako isimamie kuhakikisha kuwa wabunge wote wanatoa mikataba ya
ajira kwa
madereva wao,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
No comments:
Post a Comment