Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
YANGA leo itakuwa mwenyeji wa Azam FC katika mechi ya raundi ya nane
ya Ligi Kuu bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Timu zote zinashuka dimbani zikiwa na pointi 13 kila moja zikitofautiana kwa uwiano wa mabao.
Mechi ya leo ni ya pili kukutana kwa timu hizo msimu huu, baada ya
ile ya Ngao ya Jamii iliyofanyika mapema Septemba na Yanga kuibuka na
ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na aliyekuwa mchezaji wao Geilson
Santos ‘Jaja’ na Simon Msuva.
Katika historia ya kukutana kwao kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, Yanga
wanaonekana kuwazidi Azam baada ya msimu wa mwaka 2012/2013 kuwafunga
bao 1-0. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Aidha, katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi msimu uliopita Azam
iliifunga Yanga mabao 3-2 wakati kwenye mchezo wa pili walitoka sare ya
mabao 2-2.
Hivyo mechi ya leo inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kwani ni wazi
kuwa mabingwa watetezi Azam watataka kulipiza kisasi huku Yanga wakitaka
kuendeleza ubabe.
Yanga inaingia uwanjani ikiwa imefanya mabadiliko kwenye benchi lake
la ufundi kwa kumtimua kocha Marcio Maximo aliyeanza kuifundisha timu
hiyo tangu mwanzoni mwa msimu na kuwarejesha Hans van der Pluijm na
Charles Mkwasa.
Kwa upande wa Azam Fc Joseph Omog bado anaendelea kushika usukani
huku kocha msaidizi wake akiwa ni George ‘Best’ Nsimbe raia wa Uganda
aliyechukua mikoba ya Kally Ongala.
Kila timu ilifanya usajili katika dirisha dogo ambapo Azam
iliwasajili beki wa Ivory Coast, Paschal Wawa lakini pia winga wa
kimataifa wa Uganda Brian Majwega wakati Yanga ikiwaongeza Amis Tambwe,
Mliberia Kpah Sherman, na Danny Mrwanda.
Timu zote zilikuwa katika maandalizi ambapo Azam ilikuwa Uganda na Yanga ilienda Bagamoyo.
Makocha wote wametamba kuibuka na ushindi leo, kocha Omog akisema
hakuna cha kuizuia kuifunga Yanga huku kocha Pluijm akitamba kutumia
mfumo wa ushambuliaji na kuhimiza wachezaji wake kujiamini ili kuibuka
na ushindi.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment