Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akijiandaa
kuusaini mpira ulioshikiliwa na mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa (kulia)
MWAMUZI aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe2
Jonesia Rukyaa ni
miongoni mwa waamuzi wa kike sita waliopata beji ya Shirikisho la Soka
la Kimataifa (FIFA).
Jonesia alimudu vyema kuchezesha mchezo huo uliochezwa Uwanja wa
Taifa Desemba 13, mwaka huu na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya Yanga.
Wengine waliopata beji hiyo ni Florentina Zablon wa Dodoma na Sophia
Ismail wa Mara (Waamuzi wa kati) na Hellen Mduma wa Dar es Salaam, Kudra
Omary wa Tanga, Grace Wamala kutoka Kagera na Dalila Jaffary wa
Zanzibar (Waamuzi Wasaidizi).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Kwa mujibu wa taarifa ya kwenye mtandao wa Fifa kwa upande wa wanaume
Israel Mujuni wa Dar es Salaam, Waziri Sheha wa Zanzibar, Martin Saanya
wa Morogoro na Mfaume Nassoro wa Zanzibar wamepata beji hizo kama
waamuzi wa kati.
Samwel Mpenzu wa Arusha, John Kanyenye wa Mbeya, Fredinand Chacha wa
Mwanza, Josephat Bulali wa Dar es Salaam, Sudi Lila na Frank Komba wa
Pwani wakipata beji hizo kama waamuzi wasaidizi.
Tanzania imepata beji nyingi za FIFA kwa upande wa wanawake msimu
mpya wa mwaka 2015 kwani haijawahi kupata beji zaidi ya nne tangu ianze
kutoa waamuzi wa kike, mwaka huu 2014 haikuwa na mwamuzi wa kike wa
FIFA.
Waamuzi wa kike ambao walishawahi kuwa na beji za FIFA kuanzia mwaka
2006 ni Flora Kashaija, Isabela Kapera na Judith Gamba kama waamuzi wa
kati na waamuzi wasaidizi ni Zahara Mohamed, Saada Tibabimale na Mwahija
Omary kutoka Zanzibar.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment