Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Willbrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete asitumie kivuli cha mapumziko
ya sikukuu kuchukua uamuzi dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo anayehusika katika kashfa ya fedha za Akaunti ya
Tegeta Escrow ya Sh306 bilioni.
Pia, amemtaka Rais Kikwete kuwaeleza ukweli
Watanzania kuhusu kigogo wa Ikulu aliyenufaika na mgawo wa fedha, Sh800
milioni za akaunti hiyo zilivyotumika na mnufaikaji alikuwa nani.
Dk Slaa aliyasema hayo jana katika mkutano wa
hadhara wa kuwashukuru wananchi wa Somangila-Kigamboni Wilaya ya Temeke
jijini Dar es Salaam kwa kuwachagua wenyeviti sita kati ya 13 wa Ukawa
wa kata hiyo yenye mitaa sita.
“Tunamtaka haraka Rais Kikwete amfukuze kazi
Profesa Muhongo, asiseme anakula ‘bata’ Msoga (Kijijini kwake Bagamoyo
mkoani Pwani) eti sikukuu...Tumemchagua atusimamie na kutuongoza kwa saa
24 kwenda kula Krismasi huku wagonjwa wanakufa hospitalini ni dharau
kwa Watanzania,” alidai.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Rais ni mtumishi wa Watanzania, wachache hawawezi
kunufaika na mabilioni hayo huku wengi wanaendelea kusota na ugumu wa
maisha...Unakulaje ‘bata’ wakati Watanzania kila kona wanataka uchukue
uamuzi kwa masilahi ya Taifa, hiyo ‘bata’ kweli au ndiyo msemo unaosema
ukimwaga mboga mimi ninamwaga ugali anamwogopa Muhongo kumwajibisha?”
alisema Dk Slaa.
Alisema kumfukuza kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka pekee hakutoshi, huku
wengine waliofanya makosa kama hayo bado wanaendelea kuzunguka mitaani.
“Huyu Tibaijuka ametolewa kafara tu, kuna kigogo
wa Ikulu ambaye anaratibu shughuli za Ikulu za nchi nzima (jina
tunalihifadhi) alipewa Sh800 milioni lakini yeye hajaguswa, sasa Rais
Kikwete atueleze kwa nini alimchukulia hatua Profesa Tibaijuka na huyu
kigogo wake amemwacha kuna nini hapa kinachoendelea,” alisema Dk Slaa.
Akizungumza na wazee wa Dar es Salaam Desemba 22
mwaka huu, Rais Kikwete alisema amemweka kiporo waziri huyo hadi
atakapopata ufafanuzi wa mambo kadhaa na kwamba atakapojiridhisha
ataujulisha umma.
Dk Slaa alisema, “Rais Kikwete anatumia maneno ya
yasiyofaa katika jambo lenye masilahi mapana, kumweka kiporo kisheria au
utawala bora halipo na mimi kwa miaka zaidi ya 60 nimekuwa Padre,
Mbunge kwa miaka 15 na sasa mtumishi wa umma sijawahi hata siku moja
kusikia mtu badala ya kuchukulia hatua anawekwa kiporo.”
Juzi, Ikulu kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue alisema suala la Profesa Muhongo litatolewa uamuzi
wakati wowote baada ya mapumziko ya sikukuu.
Rais Kikwete bado hajakamilisha kulishughulikia
suala hilo na kwamba litakapokuwa tayari wananchi watajulishwa hatua
alizozichukua.
“Unakumbuka Rais alichosema? Bado analifanyia
kazi, atakapomaliza tu mtajulishwa, sasa hivi ni kipindi cha sikukuu,”
alisema Sefue. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Katika mkutano huo, Dk Slaa alisema, “Hamkukosea kuwachangua
wenyeviti wa Chadema wanaotokana na Ukawa kwani dhamira yetu ni
kuhakikisha tunaitoa CCM madarakani mwaka 2015 na hii ilikuwa njia tu.”
Aliongeza: “Ninyi viongozi hakikisheni mnatekeleza
yale mliyoyaahidi kwani kutokufanya hivyo mtakuwa mnakichimbia kaburi
Chadema mwakani.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment